Wawili wafariki dunia kwa kujinyonga Njombe

03Dec 2021
Elizabeth John
Njombe
Nipashe
Wawili wafariki dunia kwa kujinyonga Njombe

WATU wawili wamefariki dunia kwa kujinyonga akiwemo mtoto mwenye umri wa miaka 13 muhitimu wa darasa la saba mwaka huu mkazi wa mtaa wa uhuru Kata ya Maguvani mkoani Njombe mara baada ya kuonywa kuhusu upotevu wa fedha katika duka la baba yake.

Kamanda wa Polisi mkoani Njombe Hamis Issah.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani  humo Hamis Issah, amesema tukio hilo limetokea Desemba moja majira ya saa tatu huko Makambako baada ya mtoto huyo kukutwa amejinyonga katika eneo la jikoni kwa kutumia kamba ya manila.

Kamanda Issa amesema kwamba mtoto huyo baada ya kumaliza mtihani wa darasa la saba baba yake alimuachia duka akawa anauza eneo la sokoni Makambako.

"Kilichotokea cha ajabu ni kwamba baba katika kuangalia mahesabu ya duka aliona hayaendi vizuri na usiku wa tarehe moja alimuonya mtoto huyo kwamba kama anachukua pesa hizi usiendelee kuzichukua" 

"Mtoto huyu kitendo kile kilimkasirisha na matokeo yake akachukua maamuzi ya kujinyonga na amekutwa asubuhi ya tarehe mbili akiwa amejinyonga eneo la jikoni kwa kutumia kamba ya manila.Dada yake alimuona na alitumia kisu kukata hiyo kamba bila ya mafanikio yoyote kwa sababu alikua anataka kumuokoa ndugu yake na walivyokua wakimkimbiza hospitali ya nazalet iliyopo hapa hapa Makambako mtoto huyu alifariki dunia" amesema Kamanda huyo.

Wakati huo huo mtu mmoja ambaye hajajulikana kwa majina anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 60 amekutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya mti ndani ya msitu wa miti ya kupandwa huko katika kijiji Ikando kata ya Kichiwa wilayani Njombe.Tukio hilo limetokea Novemba 2, 2021 majira ya saa 12 jioni huko kijiji cha Ikando.Pia amewataka vingozi wa dini,viongozi wa mila taasisi mbalimbali kutoa elimu na kukemea maamuzi ya watu kujichukulia sheria mikononi

Habari Kubwa