Wazanzibar waliooa Mombasa wapigwa 'stop' kurudi kisa corona

01Apr 2020
Rahma Suleiman
ZANZIBAR
Nipashe
Wazanzibar waliooa Mombasa wapigwa 'stop' kurudi kisa corona

Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamad Rashid Mohammed amewataka baadhi ya wanaume ambao wameoa wake wawili Mombasa na Zanzibar kubaki huko huko nchini Kenya ili kudhibiti maambukizi ya corona.

Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamad Rashid Mohammed.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 1,2020 amesema kuwa wapo baadhi ya wanaume hasa Kisiwani Pemba wanawake wawili mmoja yupo Pemba na mwengine Mombasa nchini Kenya lakini hivi sasa wanakimbilia kurudi Pemba baada ya kuona hali mbaya ya ugonjwa huo.

Amesema wananchi 710 wamekamatwa Kisiwani Pemba wakitokea Kenya ambao wamepita katika bandari bubu.Aidha amewataka wananchi kuepuka mikusanyiko na kuacha tabia ya kunywa kahawa katika baraza za kahawa.

"Huu si muda wa kunywa kahawa barazani niwaombe wananchi wabaki ndani wanywe kahawa majumbani mwao na kwa sasa watu 304 wapo katika karantini kwa ajili ya kuchunguzwa ugonjwa baada ya kuonyesha dalili za virusi vya corona.

Habari Kubwa