- chanjo hiyo ili kuweza kusaidia Jamii kuwa na kizazi cha watoto ambao hawana ulemavu unaotokana na ugonjwa wa polio .
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Thomas Apson wakati akizindua Zoezi la chanjo ya polio katika Wilaya hiyo,uzinduzi umefanyika katika Kijiji cha Matadi Kilichopo kata ya Ndument Wilayani hapo .
Kwa mujibu wa Apson amesema mara nyingi kunapokuwa na chanjo maana yake kuna ugonjwa mbaya unaoweza kuathiri Jamii na ugonjwa huo hauna tiba.
"Niwaombe wazazi na walezi wote katika Wilaya Hii muhakikishe watoto wanapatiwa chanjo hii kwani itatusaidia tuwe na kizazi cha watoto ambao hawana ulemavu ,kwani ugonjwa wa polio hauna dawa na unaweza kumsababishia mtoto ulemavu asipopatiwa chanjo ya poli kwani dawa ya ugonjwa huu ni kuchanja tuu" amesema Apson
Hata hivyo Apson amesema kuwa Kama tunavyofahamu ugonjwa wa polio usipochanjwa kuna nafasi kubwa ya kupata ulemavu kwani kirusi hicho hakina dawa,ambapo amesema chanjo ya polio inatolewa Nchini baada ya Nchi Jirani ya Malawi kuibuka ugonjwa wa polio ,ndipo Rais wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alipotoa maagizo kuwa watoto chini ya miaka mitano wapatiwe chanjo ya polio ili kuweza kuzuia ugonjwa huo na kuimarisha Kinga za watoto .
Aidha amesema yeyote asiyetaka kuleta mtoto kwaajili ya kuchanjwa polio anamapungufu kwasababu atakuwa yupo tayatari mwanae apate ulemavu unaotokana na ugonjwa wa polio na atakuwa hana nia nzuri.
Tumeona tufanye hatua hizi za kuwapa watoto chanjo ya polio ili kuhakikishe kuwa tunailinda nchi yetu na kulinda kizazi cha watoto wetu Sasa mtu asipoleta mtoto apewe chanjo hii ana nia ovu itabidi tuchukue hatua za ziada za kinidhamu ili aweze kuleta mtoto apatiwe chanjo hiyo.
Wananchi wote wenye watoto chini ya umri wa miaka mitano waendelee kuwaleta watoto wao waweze kuchanjwa chanjo ya polio ili Taifa letu liwe salama ,nguvu kazi yetu iwe salama ili jamii yetu izidi kuwa salama .
Kwaupande wake Mganga mkuu wa Hospital ya Wilaya ya Siha Peter Mahuu amesena Juzi ( May 18 2022) wamechanja watoto 460, malengo katika Wilaya waliyopewa ni kuchanjwa watoto chini ya miaka mitano ,ni kuchanja watoto elfu 27000, kwa wilaya nzima ya Siha kwamaana hiyo kwa kila siku wanatkiwa kuchanja watoto wasiopungua 6000 ,
May 18,2022 katika Wilaya nzima ya Siha walichanja watoto 6950 ,kwahiyo tulivyuka Yale malengo ya Siku kwa hiyo tunaamini malengo yetu tuliyopewa ya Kuchanja watoto elf 27000 yatatimia."alisema Mahuu
Kata hivyo Mahuu alisema zoezi hill la chanjo ya polio linatolewa kwa muda wa Siku nne katika Wilaya hiyo na limeanza kutolewa May 18/2022,na linatarajiwa kumalizika May 21.2022 Siku ya jumamosi