Wazazi waaswa kupeleka watoto shule

20Oct 2021
Zanura Mollel
Longido
Nipashe
Wazazi waaswa kupeleka watoto shule

MKUU wa Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha Nurudin Babu amewataka wazazi kuhakikisha watoto wenye umri wa kuanza shule kupelekwa shule na wale watakao kiuka agizo hilo atawachukulia hatua za kisheria.

Akizungumza na wazazi kutoka maeneo mbalimbali waliohudhuria mahafali ya saba katika Sekondari ya Tingatinga iliyopo tarafa ya Enduiment,alisema imebainika watoto wengi wanaoanza shule kutofikia malengo yao kutokana na utoro.

" Utoro huu unatokana na watoto kuacha masomo na kukimbilia nchi jirani ya Kenya kwa ajili ya kufanya kazi,mtoto yeyote mwenye umri chini ya miaka 18 anayesoma ni marufuku kuacha masomo,ila ambaye hayupo kwenye umri wa masomo akitaka kwenda popote aende " alisema Babu.

Katika hatua nyingine akijibu matatizo yanayoikabili shule hiyo ikiwemo ukosefu wa uzio,alisema atafanya mazungmzo na uongozi wa Tanapa pamoja na Katibu Mkuu wizara ya Maliasili ilikuweza kuwaomba kupitia fedha za ujirani mwema ziweze kusaidia ujenzi wa shule hiyo iliyopo kwenye hifadhi na mapitio ya wanyamapori.

Mkuu wa shule Pantaleo Paresso alisema wahitimu hao walianza masomo wakiwa 297 lakini Leo wapo 271 na sabbu kubwa ni utoro na wengine kuhama.

" Hali ya ufaulu kwa miaka miwili ya nyuma ilikua nzuri ,2019 tulifaulisha kwa asilimia 87 ,2020 asilimia 94 na tunatarajia mwaka huu kufaulisha kwa asilimia 100"alisema Paresso.

Alisema shule hiyo inatarajia kutoa mafunzo ya technolojia (ICT) jengo na vifaa vimeshakamilika kwa gharama ya Million 103, lakini tatizo lililopo hakuna mwalimu wa TEHAMA.

Asilimia 100 shule za sekondari wilayani hapa ni za bweni,lakini hazina uzio na mazingira ya shule hizo ni magumu yapo Kenya maeneo yenye wanyama wakali hivyo Hali ya kiusalama kwa wanafunzi na walimu ni ndogo,Kilio kikubwa Cha wazazi ni serikali kutafuta wadau wa idara za Maliasili na utali kuweka uzio.

Mbunge wa Jimbo hilo Dkt Steven Kiruswa aliwahi kusema katika jitihada za kuhakikisha uzio unapatikana kwa shule hizo ,amepata mbegu ya mchongoma ya muda mfupi itakayoweza kuoteshwa kuzunguka mipaka ya shule ili kuwa na uzio wakati serikali ikijipanga kujenga uzio lmara zaidi.

Habari Kubwa