Wazazi wanaopeleka watoto shule binafsi watakiwa kutoa taarifa mapema

13Jun 2021
Na Mwandishi Wetu
Nipashe Jumapili
Wazazi wanaopeleka watoto shule binafsi watakiwa kutoa taarifa mapema

​​​​​​​SERIKALI imewataka wazazi wenye watoto waliopata ufaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwenye shule za serikali kuhakikisha wanatoa taarifa za watoto wao mapema kuwa hawata jiunga na shule hizo kwa kuwa wapo wanafunzi ambao wamefaulu na hawajapata nafasi za kujiunga-

Waziri ummy Mwalimu.

-na shule za serikali.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ummy Mwalimu,wakati akiongea na Wananchi wa Kata ya Ziba katika shule ya sekondari Ziba, amesema jumla ya wanafunzi 86,896 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano lakini wanafunzi takibani 3,800 wamekosa nafasi ya kujiunga na kidato cha tano kutokana na uhaba wa nafasi hizo, hivyo itakuwa vema kama wazazi na walezi wa wanafunzi waliopata nafasi kwenye shule za Serikali lakini hawataki kuwapeleka watoto wao huko watoe taarifa ili wale waliokosa nafasi wapate kuendelea na masomo kidato cha tano.

“Ninachotaka kusisitiza kwa wazazi na walezi kwa sababu tuna wanafunzi kama 3,800 ambao hawajapata ya kuendelea na elimu ya kidato cha tano, kwa hivyo kama mzazi au mlezi ameshafanya maamuzi ya kumpeleka mtoto wake kwenye shule ya sekondari binafisi tunaomba ajaze fomu katika mfumo wetu ili aweze kuiachia nafasi hii kwa vijana ambao wamefaulu lakini wamekosa nafasi” amesema Waziri ummy Mwalimu.

Katikati ya mazungumzo yake, pia Waziri Ummy ameahidi kupeleka fedha kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa bwalo la kulia chakula katika shule hiyo ili kuondoa kero inayowakabili wanafunzi wa shule hiyo.

 

Habari Kubwa