Waziri atishia kuifuta NFRA wakishindwa kununua tani tano ya mazao

14Mar 2019
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe
Waziri atishia kuifuta NFRA wakishindwa kununua tani tano ya mazao

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ameitishia kufuta Wakala wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA), kama hautakuwa na uwezo wa kununua tani laki tano za mazao kwa wakulima.

WAZIRI wa Kilimo Japhet Hasunga.

Hasunga ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizindua mashine maalum ya kusafisha mahindi iliyotolewa na Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kwa NFRA, jijini Dodoma. 

Amesema kuna mabadiliko makubwa yanayokuja kufanyika NFRA, kwa kuwa sio kazi yao kuhifadhi tu chakula bali lazima wanunue mazao yote ya ziada kwa wananchi na wakauze.

“Nimewashangaa mpo kwa ajili ya kuhifadhi eti chakula cha Taifa, wakati mazao yapo kwa wananchi badala ya kwenda kutafuta masoko mkayanunue mazao yaliyopo kwa wakulima, kuna masoko kama nchini Misri nendeni mkatafute masoko,”amesema.

Kufuatia hali hiyo, Hasunga ametaja mambo matatu yanayotakiwa kufanyika na NFRA ili isifutwe.

“Jambo la kwanza lazima muwe na uwezo wa kununua tani laki tano kama hamna uwezo nitafuta NFRA, nunua na kuuza  si kuhifadhi tu, sio mnakaa hapa hata kutafuta masoko hamtafuti,”amesema.

Waziri Hasunga amesema jambo la pili ni lazima wawe na maghala ya kuhifadhi vizuri mazao kwa miaka mitano kutokana na kwasasa yaliyopo yanaweza kuhifadhi kwa miaka miwili au mitatu tu baada ya hapo yanakuwa yameharibika.

Habari Kubwa