Waziri Gwajima ataka watoto kupewa elimu ya ufundi stadi

20Jan 2022
Na Mwandishi Wetu
Dodoma
Nipashe
Waziri Gwajima ataka watoto kupewa elimu ya ufundi stadi

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima, amewataka wakuu wa taasisi za ustawi wa jamii na vyuo vya maendeleo ya jamii kuanzisha mpango maalum kwa ajili ya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili wapate elimu ya ufundi stadi itakayowasaidia kujiendeleza kiuchumi.

Dk. Gwajima amebainisha hayo jijini Dodoma wakati akizungumza katika makao ya taifa ya watoto yaliyopo Kikombo na amesema taasisi na vyuo vinatakiwa kuwa chachu ya maendeleo kwa jamii ili kutatua changamoto zilizopo.

Kwa upande wake, naibu waziri wa wizara hiyo, Mwanaidi Ali Khamis, pamoja na na katibu mkuu wake, Dk. Zainabu Chaula, wamewaasa maafisa ustawi wa jamii katika makao ya taifa ya watoto Kikombo wahakikishe wanatoa malezi bora kwa watoto ili waweze kuchangia maendelo ya uchumi wa taifa kupitia taaluma watakazopata.

Afisa mfawidhi wa taifa wa watoto, Vivian Kaiza, amesema kuwa atafuata miongozo na maelekezo ya serikali katika ufundishaji kwa lengo la kuwajengea uwezo watoto ili kushawishi wengine wanaoishi katika mazingira hatarishi mitaani wajue umhimu wa kufanya kazi za kujipatia kipato.

Habari Kubwa