Waziri Kalemani awapa mtihani vigogo Simanjiro

18Oct 2019
Dotto Lameck
Dar es Salaam
Nipashe
Waziri Kalemani awapa mtihani vigogo Simanjiro

WAZIRI wa  Nishati  Dkt Medard Kalemani amewataka Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Mameneja wa Tanesco wilayani Simanjiro mkoani Arusha kuwahamasisha wananchi waliopo katika wilaya zao kulipia umeme ili waweze kuwafunga katika kata zao zote.

Kalemani amesema hayo wakati akiongea na wananchi wa Kijiji cha Naepo Kata ya Naisinyai wilayani Simanjiro mkoani Manyara ambapo mbali nakuongea na wananchi hao pia alizindua mradi na kuwasha umeme katika Shule ya Msingi Naepo pamoja na Shule ya Sekondari ya Shambarai zilizopo katika wilaya hiyo. 

Hata hivyo Kalemani amesema kuwa anafahamu katika kijiji cha Naisinyai na vijiji jirani vimepata umeme lakini bado haujatosheleza na hivyo anafuatilia katika vijiji ambavyo havina umeme na hatahakikisha vinapata Umeme. 

"Napenda kutoa maelekezo kwa Mkandarasi pamoja na Tanesco Wilaya ya Simanjiro, ikifika November 16 mwaka huu vijiji vyote pamoja na kaya zote za Naisinyai viwe vimepatiwa umeme, na maanisha Kitongoji cha Naepo kiwekimejaa umeme kambi ya Chokaa kulipelekwa umeme lakini bado ujaja sasa napenda kukwambia Mkandarasi kabla ujatoka hapa uakikishe kaya zote, vijiji vyote pamoja na Kitongoji cha Kibaoni kiwe kimejaa umeme.,"amesema Kalemani 

Aidha amemtaka Mkandarasi ambaye ni Angelique International Ltd kwa kushirikiana na Tanesco Wilaya ya Simanjiro na Mkoa wa Manyara kwa ujumla kuhakikisha wananchi wote Wilaya ya Simanjiro katika vijiji vyote pamoja na vitongoji vyote vinapata umeme na sio mradi umeme tu bali ni umeme wa uhakika. 

Naye Meneja wa Tanesco Wilaya ya Simanjiro, Zakaria Masatu ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Nishati Kwa kuendelea kuwa karibu na Shirika katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali na hivyo kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya maendeleo ya wananchi wa Wilaya ya Simanjiro na Tanzania kwa ujumla.

Habari Kubwa