Waziri Ummy amuwakilisha Rais Samia kwenye kakao cha Global Covid-19

13May 2022
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Waziri Ummy amuwakilisha Rais Samia kwenye kakao cha Global Covid-19

​​​​​​​WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu, leo Mei 13, 2022 amemuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye kikao cha pili cha ‘Global Covid-19’ kilichofanyika kwa njia ya mtandao ulioandaliwa za Serikali ya Belize, Ujerumani, Indoneaia, Senegal na Marekani.

Katika kikao hicho Waziri Ummy amesema hadi kufikia Mei 9, Mwaka huu jumla ya dozi 7,713,526 za chanjo ya UVIKO-19 zimetolewa nchi nzima na watu wapatao 4,110,884 ambao ni sawa na asilimia 13.37 tayari wameshapata chanjo hiyo ambayo makadirio yake ni kuchanja watanzania wapatao 30,740,928.

Waziri Ummy amesema hadi sasa Tanzania imeshapokea dozi 11,232,374 kutoka COVAX facility pamoja na washirika wengine.

Vilevile Waziri Ummy ameeleza katika kikao hicho kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha wananchi wanapata Chanjo dhidi ya UVIKO-19 ikiwemo kutoa elimu ya umuhimu wa chanjo kwa kuwa hatujui wimbi jingine la Kirusi litakuaje.

Habari Kubwa