Waziri Ummy aridhishwa ujenzi wa jengo la utawala Kibiti

16Sep 2021
Na Mwandishi Wetu
KIBITI
Nipashe
Waziri Ummy aridhishwa ujenzi wa jengo la utawala Kibiti

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu ameridhishwa na Ujenzi wa jengo la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani.

Akikagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa  na Halmashauri  ya Wilaya ya Kibiti leo Waziri Ummy ametoa siku 30 kukamilisha ujenzi uliobak na watumishi wa Halmashauri hiyo kuhama katika Ofisi hizo

Waziri Ummy ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti kuhakikisha inatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za wakuu wa Idara

Aidha Ujenzi wa Jengo la Utawala lhadi kukamilika  unakadidiwa kugharimu kiasi cha shilingi  bilioni 5.6 na mpaka Sasa ujenzi umekamilika kwa asilimia 98