Ndaki alitoa maagizo hayo jana, akiwa wilayani Mbarali mkoani Mbeya wakati akizungumza na wakulima na wafugaji katika Bonde la Usangu.
Alisema serikali inahitaji ranchi zote zilipe madeni kuanzia Januari 12 hadi Februari 15, mwaka huu na kwamba zitakazoshindwa kulipa, zinyang’anywe na kupewa wawekezaji wengine.
Pia alipiga marufuku kufanyika kwa shughuli za kilimo kwenye maeneo ya ranchi kwa madai kuwa ni kwenda kinyume cha makubaliano ya mkataba.
"Nimetoa muda wa kuanzia Januari 12 hadi Februari 15 majira ya saa saba mchana, Bodi ya NARCO iwe imekusanya madeni yote wanayoyadai kwenye ranchi mbalimbali nchini, lakini pia wawekezaji kufuata makubaliano ya mikataba ili kila upande unufaike na ranchi hizo," alisema.
Katika hatua nyingine, Ndaki aliwahakikishia wawekezaji katika wa ranchi mbalimbali nchini kwamba serikali imewaandalia mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao na kuomba waendelee kushirikiana.
Soma zaidi; https://epaper.ippmedia.com