Wenye viwanda wataka ndege kusafirisha minofu ya samaki

26May 2020
Neema Emmanuel
MWANZA
Nipashe
Wenye viwanda wataka ndege kusafirisha minofu ya samaki

Wamiliki wa viwanda vya kuchakata minofu ya samaki waiomba serikali kuongeza ndege za kubeba mizigo mara kwa mara nchini ambayo itasafarisha mizigo nje ya nchi ili kukuza biashara na kuboresha ubora wa bidhaa wanayosafirisha.

ndege ya Rwanda A330-300 yenye usajili 9XR-WP ikipakia minofu ya samaki.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Kiwanda cha Nature’s Fish Limited, Ashok Vannadil alipokuwa akiishuhudia mzigo wake wa minofu ya samaki ukisafirishwa kuelekea Brussels nchini Ubelgiji kupitia Ndege ya Rwanda A330-300 yenye usajili 9XR-WP.

Amesema kuwa ni wakati wa serikali kuongoze usafiri kwani tayari fursa zimeanza kufunguka kwa sababu mzigo unapofika kwa wakati katika soko kutaongeza ubora wa bidhaa na bei kuwa juu.

“Tunaishukuru serikali kwa kuboresha biashara ya samaki kwa kuboresha uwanja huu, Mwanza ni Jiji la samaki tunahitaji ndege mara kwa mara ili kuboresha bidhaa zetu  hii ni mara ya kwanza kwetu lakini tutaundendea haki uwanja huu kwa kufanya kazi ipasavyo”amesema Vannadil.

Naye Meneja uzalishaji kutoka Kiwanda cha Tanzania Fish Processors Limited, Dhanapal Gurisamy, amesema ni mara ya tatu kampuni hiyo inasafirisha mzigo kwenda Ulaya na kwamba zoezi hilo lina kwenda vyema na wananufaika na kufaidi matumzi ya uwanja wa Ndege Mwanza kwa kupata huduma bora.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, akiwa uwanjani hapo kushuhudia awamu ya nne ya kupakia minofu ya samaki kwenda Ulaya, amesema serikali imewekeza vya kutosha na lengo la Rais ni Tanzania Dk. Magufuli ni kufikia uchumi wa kati wa viwanda hivyo leo ndege hiyo imesafirisha tani 22 za minofu ya samaki ambapo mafanikio yaliopo kwa sasa ni makubwa kwani wawekezaji wanapata faida kubwa.

Amesema kuwa kuna mashirika yameanza kuonyesha dalili za kuja nchni kuchukua bidhaa hizo na kusisitiza kuwa huo ndio wakati wa kuonyesha ubora wa bidhaa serikali inapofanya uimalishaji na uboreshaji hivyo wananchi wanatakiwa kujitahidi kuchangamkia fursa hiyo na kuzalisha bidhaa zenye ubora zitakazo ingizwa kwenye soko la kimataifa.

Ameongeza kuwa kila siku kiwango cha mzigo kinazidi kuongezeka kitendo hicho kitasaidia bei ya usafirishaji unapungua kuliko mzigo unapokuwa mdogo .

“Namshukuru Rais kwa kazi kubwa anayoifanya ,Mwanza inazidi kufungua fursa nyingi kiuchumi kwa jamii na kuongeza ubora wa maisha kwa watanzania”amesema Mongella.

Habari Kubwa