"Kauli mbiu ya mwaka huu, ni "Miaka 100 ya Mahakama:mchango wa mahakama katika kujenga nchi inayozingatia Uhuru, Haki,Udugu, Amani na ustawi wa wananchi 1921-2021" amesema Temu
Amesema kuwa, jamii wilayani humu hawana uelewa kuhusu taratibu za uendeshaji wa mashauri mahakamani na kueleza ukatili wa kijinsia kwa jamii ya kifugaji bado wanawake na watoto wanafanyia vitendo vya kikatili na kunyanyasika kijinsia lakini mahakama imekua mstari wa mbele kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha jamii inapata uelewa wa kutosha juu ya madhara ya ukatili kwa wanawake na watoto.