Wizara yatoa ufafanuzi ongezeko muda wa masomo

02Jul 2020
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Wizara yatoa ufafanuzi ongezeko muda wa masomo

Wizara ya Elimu imetolea ufafanuzi ongezeko la saa 2 za masomo kwa Wanafunzi baada ya Shule zote nchini kufunguliwa ili kufidia muda ambao umepotea kutokana na mlipuko wa virusi corona.

Imesema kuwa tathmini waliyofanya imebaini jambo hilo ni gumu kutekelezeka kwasababu kuna shule zenye vibali vya kuendesha masomo kwa mfumo wa 'double shift'. Pia suala la usafiri kwa wanafunzi waishio mbali nalo limeonekana kuwa ni changamoto.

Kutokana na hilo, wizara imezitaka shule kutumia ratiba za vipindi 8 kama ilivyokuwa awali na shule zitakazoona umuhimu wa kuongeza muda wa masomo zitatumia muda uliopangwa kwenye ratiba zao.

 

Habari Kubwa