Wizara ya Elimu yawataka watumishi wake kutumia fedha za IMF vizuri

23Oct 2021
Na Mwandishi Wetu
Dodoma
Nipashe
Wizara ya Elimu yawataka watumishi wake kutumia fedha za IMF vizuri

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imetoa maelekezo kwa watendaji wa Wizara pamoja na taasisi zitakazotekeleza miradi wahakikishe maandalizi ya mpango wa matumizi ya fedha zilizotolewa na Shirika la fedha la kimataifa (IMF) yanakamilika ndani ya Octoba 30 mwaka huu-

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako.

-sambamba na kutoa mpango wa utekelezaji wa miradi itakavyofanyika.

Hayo yamesemwa leo Octoba 23,2021 jijini Dodoma na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, wakati akitoa taarifa huhusu utekelezaji wa mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya uviko 19, ambapo amewataka watendaji wa Wizara na Taasisi zilipo chini yake kuhakikisha mpango wa utekelezaji wa miradi unatolewa haraka.

Waziri Ndalichako amesema kuwa sekta ya elimu imetengewa shilingi bilioni 368.9 na Wizara ya Elimu imepata shilingi bilioni 64.9 kutekeleza miradi iliyochini ya Wizara hiyo.Amesema kuwa hadi ifikapo Octoba 30, 2021 kila taasisi itakayotekeleza mradi huo iwe imekamilisha maandalizi na mipango ya utekelezaji pamoja na kuandaa mpango kazi utakao ainisha hatua mbalimbali za taratibu za manunuzi ya huduma na vifaa.

“Hadi tarehe 30 mwezi huu kila taasisi iwe imekamilisha na iainishe lini vifaa vitanunuliwa, vifaa vyote vinunuliwe kwa kuzingatia bei ya soko nataka na mimi nikienda kununua kifaa bei iwe ndio hiyo” amesema Prof. Ndalichako.

Habari Kubwa