World Vision yasaidia shule iliyoungua

13Sep 2020
Daniel Sabuni
Mwanga
Nipashe
World Vision yasaidia shule iliyoungua

SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Kimataifa la World Vision Tanzania limetoa msaada wa vifaa vyenye thamani ya Shilingi Milioni 30 za kitanzania kwa lengo la kusaidia wanafunzi walioathirika na janga la kuunguliwa na bweni la Shule ya Sekondari Nyerere iliyopo wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Thomas Epson akimkabidhi mwanafunzi wa shule ya sekondari Nyerere Jenipher Jacob. PICHA: Daniel Sabuni

Baadhi ya msaada wa Vifaa vilivytolewa na shirika hilo ni mablanketi 120, mashuka 226, vyandarua 126, taulo za kike 390, magodoro 67, vitanda "dabo deka" 66 na madaftari 1320 (Counter book).

Picha ya bweni la wasichana wa shule ya sekondari Nyerere lililoungua hivi karibuni Wilayani mwanga Mkoani Kilimanjaro. PICHA: Daniel Sabuni 

Akizungumza wakati akikabidhi vifaa hivyo Meneja wa Kitengo cha maafa cha World Vision, Victor Katambala, amesema kutoa msaada pale majanga mbalimbali yanapotokea katika jamii ni sehemu ya majukumu ya Shirikika hilo.

Habari Kubwa