Zanzibar ni kubwa kuliko tofauti zetu asema rais mteule Dk. Mwinyi

29Oct 2020
Na Mwandishi Wetu
Zanzibar
Nipashe
Zanzibar ni kubwa kuliko tofauti zetu asema rais mteule Dk. Mwinyi
  • Atwaa zaidi ya asilimia 76 ya kura zote akifwatiwa na Maalim Seif Sharif wa ACT aliyepata asilimia 19.8 ya kura zote.

Dkt Hussein Ali Mwinyi amechaguliwa rais mpya wa Zanzibar chini ya tiketi ya CCM baada yakupata zaidi ya asilimia 76 ya kura zote. Aliekuwa mpinzani mkubwa, Maalim Seif Sharif wa ACT Wazalendo alifanikiwa kupata asilimia 19.8 ya kura zote.

Ushindi huo mkubwa ulitangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) jioni hii na mteule huyo ambaye ni mtoto wa rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akatoa hutuba fupi ya kukubali uteule huo.

"Sasa ni wakati wa kujenga Zanzibar mpya, Zanzibar mpya itajengwa na sisi sote tukifanya kazi kwa pamoja," alisema katika hotuba yake.

"Tuweke tofauti zetu pembeni, Zanzibar ni kubwa na muhimu kuliko tofauti zetu ," aliongeza rais mteule.

"... tusherehekee kwa heshima kwa wote, hakuna mshindi bila mshindani ... uchaguzi umemalizika sasa tufanye kazi ya kujenga nchi yetu," alisema.

Matokeo ya uchaguzi 2020 yanaendelea kutoka, usipitwe endelea kutufuatilia: https://epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa