Zitto atangaza atakapogombea, aripoti Polisi, aungana na Seif

20Jul 2020
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Zitto atangaza atakapogombea, aripoti Polisi, aungana na Seif

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini anayemaliza muda wake Zitto Kabwe, ametangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo hilo kwa mara nyingine tena.

Zitto Kabwe.

Kupitia Ukurasa wake wa kijamii wa ‘twitter’ Zitto ameandika kuwa huu ndio wakati muhimu kwa historia ya demokrasia na yuko tayari kugombea ubunge Kigoma mjini.

“Huu ni wakati muhimu zaidi katika historia ya demokrasia ya Vyama vingi nchini. Ni wakati wa kuhami demokrasia yetu. Ni wakati wa kuhakikisha tunaunda Serikali ili kurejesha furaha kwa Watanzania. Nimeamua kuwa Nitagombea Ubunge Kigoma Mjini”, ameandika Zitto.

Wanachama ambao wametia nia mpaka sasa katika jimbo hilo ni Zitto Kabwe, Abdul Nondo, Hussein Kaliango na Idd Adam.

Wakati huo huo Kiongozi huyo wa ACT leo Julai 20, 2020 ameripoti katika kituo cha Polisi Lindi kwenye kesi ya kuhatarisha amani wakati akiwa katika ziara yake ya Jimbo la Kilwa Kusini.

"Tumeripoti Polisi Lindi na kuelekezwa kurudi tena tarehe 10/08/2020. Polisi wanasema kuwa wanaendelea na upepelezi wa tuhuma dhidi yetu kwamba tumehatarisha Amani huko Kilwa. Baada ya kuripoti nimeungana na Mwenyekiti wa Chama Maalim Seif Katika Ziara ya Mkoa wa Selous (Chabruma)." ameandika kwenye mtandao wake wa twitter

 

Habari Kubwa