Zitto, Bwege watinga tena polisi

02Jul 2020
Na Mwandishi Wetu
Kilwa
Nipashe
Zitto, Bwege watinga tena polisi

KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, na viongozi wengine saba wameripoti kituo kikuu cha polisi Lindi kama walivyotakiwa na Jeshi la Polisi.

Kiongozi huyo na mbunge wa Kilwa Kusini, Suleiman Bungara, maarufu kama Bwege, pamoja na wengine, walikamatwa Juni 23, mwaka huu, kwa madai ya kuhatarisha amani.

Jana, baada ya kuripoti walitakiwa kurudi tena Julai 20, mwaka huu, huku chama hicho kikilalamikia usumbufu kwa kiongozi wao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Naibu Katibu wa Kamati ya Habari, Uenezi na Uhusiano kwa Umma, Janeth Rithe, chama hicho kitaendelea na shughuli zake za kisiasa bila kujali usumbufu.

“Licha ya vitisho vya mara kwa mara kutoka kwa jeshi la polisi, jana Kabwe amerejea Kilwa kuwapokea madiwani na kufanya kikao na viongozi na wanachama wa ACT,” alisema.

Alisema ziara hizo ni endelevu katika maeneo mbalimbali nchini na kuwaomba wanachama wao kuendelea kuwaunga mkono.

Habari Kubwa