Kerr aidai Simba mamilioni

15Jan 2016
WAANDISHI WETU
Nipashe
Kerr aidai Simba mamilioni
  • Muingereza huyo amekuwa kocha wa 21 kutimuliwa Simba tangu 1998 vurugu za kufukuza ovyo makocha zilipoanza Msimbazi ...

SIMBA inatakiwa kumlipa Dylan Kerr Sh. milioni 21.3 kutokana na uamuzi wa klabu hiyo kuvunja mkataba wake na kocha huyo.

Kocha wa Simba, Dylan Kerr

Jumatatu klabu hiyo ilitangaza kuachana na Muingereza huyo aliyetua Msimbazi Julai mwaka na kuiongoza timu yao katika mechi 13 za Ligi Kuu, akishinda nane, sare tatu na kupoteza mbili kwenye nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi hiyo msimu huu.
Rais wa Simba, Evans Aveva, aliambia Nipashe kwa simu jana kuwa kocha huyo ambaye tayari wameshamkabidhi tiketi ya ndege ya kurejea Uingereza, anawadai dola za Marekani 10,000 (Sh. milioni 21.3) ambazo ni mishahara ya miezi miwili, Desemba na Januari.
"Hatuna kitu kingine tunachodaiwa na Kerr zaidi ya mshahara wa mwezi Desemba na mwezi huu ambao tumekatisha mkataba wake," alisema Aveva.
Kerr (48), Muingereza wa pili kuzinoa Simba na Yanga tangu 1997 Steve McLennan alipofundisha Jangwani, amefungashiwa virago baada ya kukaa Msimbazi kwa miezi sita alipochukua mikoba ya Mserbia Goran Kopunovic.

Habari Kubwa