Aidha, Azaki imewataka viongozi wanaohusika na majadiliano hayo, watumie siku ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwatangazia wananchi hatma ya mgogoro huo.
Akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Ismail Jussa Ladhu, alisema Maalim Seif atazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu hali ya kisiana visiwani humo kwa ujumla.