Majaliwa mgeni rasmi Dodoma marathon

25Jan 2016
Nipashe
Majaliwa mgeni rasmi Dodoma marathon

Waziri Mkuu Majaliwa Kasim Majaliwa anatarajiwa kuzindua mbio za nusu marathon zitakazojulikana kama 'Dodoma Hapa Kazi Tu' zitakazo Jumamosi na kushirikisha wanariadha zaidi ya 5000 imeelezwa.

Waziri Mkuu Majaliwa Kasim.

Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka, alisema licha ya mbio hizo kuwa na lengo la kukuza vipaji lakini ni sehemu ya maandalizi wanariadha wa watakaokwenda kushiriki katika Michezo ya Olimpiki inayotarajiwa kufanyika Agosti mwaka huu nchini Brazil.

Mtaka alisema mbio hizo zitafanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma na kueleza pia zitawahusisha wanariadha wawili ambao wameshafuzu kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil.

Alisema mbio hilo zimegawanyika katika makundi matatu ambapo kundi la kwanza litakimbia umbali wa kilomita 2.5 na lingine litachuana katika kilomita tano huku akiongeza kwamba watashirikisha na wanamichezo wenye mahitaji maalumu ikiwemo walemavu, wazee na viongozi mbalimbali.

Alitaja zawadi kwa mshindi wa kwanza katika mbio za kilomita 21 ni pikipiki (wanawake na wanaume) yenye thamani ya Sh. milioni 2.8, mshindi wa pili mabati 100, mshindi wa tatu mabati 40 huku Sh. 200,000 zikienda kwa mshindi wanne.

Zawadi nyingine ni Sh. 100,000 kwa mshindi wa tano na watakaoshika nafasi ya sita hadi 10 kila mmoja atajinyakulia 50,000.