Kila glasi ya kilevi, inakukaribisha kupooza

18Apr 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Kila glasi ya kilevi, inakukaribisha kupooza

MTU anapoonja kilevi japo glasi moja, basi afya yake inakuwa jirani na shinikizo la damu, inaeleza matokeo ya utafiti wa miaka 10 iliyowahusu Waingereza na Wachina 500,000.

Kilevi katika glasi. PICHA: MAKTABA.

Katika tafsiri yake, inaelezwa vilevi mara zote vina hatari kubwa ya mtu kupata maradhi ya kupooza na suluhisho bora kwa wanywaji ni kuacha imapobidi au kutumia kiwango kidogo.

Vyuo vikuu vya Peking na Oxford, katika matokeo yao ya utafiti vimebaini mambo kadhaa, kwamba:

Wastani wa chupa moja au mbili ya bia, au kinywaji cha kiwango hicho kwa siku, inamweka mnywaji hatarini kwa asilimia 10 hadi 15.

Pia, matumizi ya chupa nne yanamsogeza zaidi katika hatari ya kiwango cha asilimia 35 ya mwili kupooza.

Mtaaluma Profesa David Spiegelhalter, kutoka Chuo Kikuu cha Cambridge, Uingereza, anasema kadri kunakuwapo ongezeko la kinywaji cha wine japo kwa nusu glasi, basi kuna uwezekano wa shinikizo la damu kwa wastani wa asilimia 38.

Pia, utafiti huo unaeleza kwamba, hakuna kiashiria cha nafuu kwamba, kunywa kidogo kunamweka mtu salama.

•Kwa mujibu wa mtandao.

Habari Kubwa