Ufugaji wa sungura umeboresha upatikanaji wa chakula bora katika kijij

21Oct 2020
WAANDISHI WETU
Dar es Salaam
Nipashe
Ufugaji wa sungura umeboresha upatikanaji wa chakula bora katika kijij

UNICEF, CUAMM na TAHEA

UNICEF, CUAMM na TAHEA

Kijij cha Mgama kilichopo halmashauri ya wilaya ya Iringa, ni mashuhuri kwa kilimo cha mazao ya chakula ambayo husafirishwa katika mikoa mbalimbali ya Tanzania. Kijiji hichi kina idadi kubwa ya watoto walio chini ya miaka mitano (725) kuliko vijiji vingine vilivyopo katika kata ya Mgama. Kaya nyingi zilizopo kijiji cha Mgama hazina uhakika wa chakula kutokana na kutopatikana kwa chakula wakati wote.

Katika juhudi za kutoa huduma za lishe, mpango unaofadhiliwa na msaada wa serikali ya Ireland umelenga kupunguza udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka miwili mkoani Iringa na Njombe. UNICEF kushirikiana na serikali ya Tanzania pamoja na mashirika ya CUAMM na TAHEA, wanatekeleza mpango wa kuwezesha uzalishaji na upatikanaji wa chakula mbalimbali katika kaya zilizopo mikoa ya Iringa na Njombe.

Sabina Pilla, 54, ni mganikazi anaeishi katika kijiji cha Mgama. Kazi yake ya uganikazi inahusisha kuwa mkulima wa mfano na kutoa elimu ya kilimo na mifugo katika kijiji anachoishi. Sabina ni kati ya waganikazi 96 kutoka mkoa wa Iringa waliopata mafunzo ya kilimo bora na ufugaji wa wanyama wadogowadogo. Mwaka 2018, alihamasisha jamii kuanzisha kikundi cha uhasihi kwa ajili ya kujifunza kuhusu Kilimo na ufugaji bora. Kikundi kiliitwa “Mtoto Kwanza” chenye idadi ya wanakikundi 25. Kikundi kilihamasishwa kuanzisha bustani za nyumbani na ufugaji wa sungura.

Katika juhudi za kutoa huduma za lishe, waganikazi wote 96 walipewa sungura wawili kwa lengo la kuwafunga wazaliane na kuwagawia walengwa wa mradi ambao ni wajawazito na kina mama/walezi wenye watoto wa umri chini ya miaka 2. Baada ya miezi 4, Sabina alikua na sungura 20 ambapo aligawa sungura 16 katika kaya 8 zilizipo katika kikundi cha “Mtoto Kwanza”. Wanakikundi 8 waliopata sungura waliendelea kufuga na kuwagawia wengine na mzunguko ukaendelea.

Kufikia Septemba 2018, kaya 56 zenye watoto zilizopo kijiji cha Mgama na kijiji cha karibu cha Ibumila zimenufanika kupata jumla ya sungura 112. Kaya 72 zilizopo katika mpango wa kupata sungura, zimeweza kuanzisha bustani za nyumbani ili kuweza kupata virutubishi vingine vilivyopo katika mbogamboga mbalilmbali. Katika mpango huu wa kugawiana sungura, kaya zilihamasishwa kuuza sungura wachache na kula wengine ili kuongeza upatikanaji na ulaji wa vyakula venye protini. Fedha iliyopatikana kutokana na mauzo ya sungura, zimetumika katika kununua mbolea kwa ajili ya kilimo cha mahindi na nyanya. Pia, mbolea ya sungura inatumika bustani za nyumbani na katika uzalishaji uyoga.

Agnes Kitime, 35, anaishi na mume wake pamoja na familia yenye watoto wanne. Agnes anaishi jirani na Sabina na pia ni mwenyekiti wa kikundi cha “Mtoto Kwanza”.  Baada ya kuhamasishwa, Agnes aliweza kufuga sungura wengi na kuanzisha bustani nyumbani kwake. Juhudi zake zilipelekea kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa kikundi. Pamoja na faida nyingine, Agnes ameweza kupangilia chakula na lishe bora katika familia yake. Baada ya kufanikiwa, Agnes anasema, “Mtoto wangu wa miaka miwili, Oliva Kalinga anapata chakula chenye lishe mchanganyiko na ameweza kukua vizuri. Anapata chakula chenye protini kinachomwezesha kukua vizuri kimwili na kiakili.”

Agnes aliendelea kusema, “Mimi pamoja na familia yangu hatukuwahi kula nyama ya sungura kabla ya mpango huu kuanza, pia sikuamini kama uzalishaji wa sungura unaweza kukuongezea kipato. Lakini kupitia kikundi chetu cha unasihi, nilijua kwamba nyama ya sungura ni tamu na nzuri kwa afya hasa kwa mtoto wangu Oliva. Watoto wangu wote sasa wanapenda sana nyama ya sungura na wamekua wakinikumbusha niwapikie nyama ya sungura.”

Habari Kubwa