Apple yajikabidhi kwa Wachina

12Jan 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Apple yajikabidhi kwa Wachina

KAMPUNI ya kutengeneza bidhaa za kompyuta na huduna nyingine za kielektroniki, kuanzia mwezi ujao itaendesha shughuli zake nchini China, chini ya uwakala wa kampuni ya Kichina, imeelezwa,

Hiyo inafanywa kama sehemu ya kuridhia vigezo, sheria na masharti ya nchi hiyo na tayari imeshawafahamisha wateja wake wa nchini humo.

Kutokana na mabadiliko hayo mpya, China kupitia kampuni wakala itakuwa na uhuru wa kuona maudhui ya vielelezo vyote vilivyomo katika data za Apple. Kampuni hiyo inasema imeamua kufanya hivyo kuridhia masharti yaliyowekewa na Wachina kupitia sheria zao.

Kwa mujibu wa sheria mpya ya Julai mwaka jana,  inayosimamia vifaa hivyo vya kielektroniki, ni kwamba kampuni hizo kuhifadhi data zake inazotumia ndani ya China.

Wakala wa Apple nchini China ni kampuni ya Cloud Big Data (GCBD), inayomilikiwa na serikali na Apple na  ilishatangaza kuhifadhi data zake zenye thamani ya Dola za Marekani bilioni moja. (Sh. Trilioni 2.2)

Ni tukio lililopokewa na mitandao ya kijamii, kwamba inatoa fursa kwa serikali kuwa na ulinzi wa kutosha kwa raia wake. 

Wakati kuna msukumo huo kutoka upande wa mtandao ya kijamii, vyombo vya habari vya serikali navyo vimekuwa vikiandika na kuripoti katika mtazamo wa kushabikia kampuni ya Apple, kujiendesha katika mazingira ta kuheshimu sheria za china.

Mwaka jana kampuni hiyo ya kigeni iliandamwa kwa fedha za kamisheni ambayo imekuwa ikipata katika uendeshaji shughuli zake, hasa kutoka mitandao ya jamii.  

Katika utetezi  wake wakati huo, Mtendaji Mkuu wa  Apple, Tim Cook, aliitetea kampuni yake alisema inafanya kazi China kwa kufuata masharti ya leseni yake nchini humo na kamwe haiendi nayo kinyume.

BBC Ends

 

Habari Kubwa