Aspirini tiba ya kiharusi cha damu kichwani

30May 2019
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Aspirini tiba ya kiharusi cha damu kichwani

WAGONJWA wanaopatwa na kiharusi kutokana na tatizo la mshipa kupasuka kichwani na kuvuja damu, tiba imepatikana.

Hiyo ni kupitia matumizi ya dawa aina ya aspirini, inayozuia uwezekano wa kuugua tena maradhi hayo au shinikizo la moyo.

Mabingwa waliotafiti, wanasema matumizi ya aspirini ni msaada mkubwa wa kuzuia uwezekano wa watu kupatwa tena na matatizo hayo kwa mara nyingine, lakini kigezo kikuu ni ushauri wa daktari kuwa jambo muhimu wakati wote.

Ni kazi mpya ya dawa hiyo, mbali na iliyozoeleka kuondoa maumivu na homa mwilini.

Sehemu kubwa ya kiharusi inachangiwa na damu kuganda katika mshipa, hivyo aspirini inasaidia kulainisha damu hiyo na inaondoa uwezekano wa kiharusi au shinikizo la damu na kiharusi.

Hata hivyo, pamoja na kushauriwa matumizi ya aspirini, kiafya imepigwa marufuku kwa yeyote mwenye umri chini ya miaka 16 kushirki matumizi hayo, isipokuwa kama mgonjwa atashauriwa na daktari.

Chama cha Kiharusi cha Uingereza kinasena, katika utafiti waliofanyiwa na kuhusisha watu 537 nchini Uingereza, ilibainika kwamba nusu ya waliojaribiwa kutumia dawa hiyo, walionyesha mafanikio.

Katika hilo, watafiti wanasema ina sifa kukabili shinikizo itokanayo na matatizo ya ubongo na wakati huo huo, ni salama kwa watumiaji.

Mtafiti kiongozi, Profesa Rutsam Salman, kutoka Chuo Kikuu cha Edinburgh, Uingereza anasema licha ya wengi kuhofu matumizi hayo, wataalamu hao watafiti, bado wanakiri kukubali uthabiti huo wanaouthibitisha.

Mtaalamu wa moyo, Profesa, Metin Avkiran, kutoka Mfuko wa Moyo wa Uingereza, ambao ndiyo wadhamini utafiti, ana maelezo kuhusu nafasi ya aspirini katika eneo lake la ujuzi wa tiba.

"Theluthi moja ya watu waliopata tatizo la kutokwa  damu ambayo pia inajulikana kama kiharusi cha damu kichwani, walifanya hivyo kwa kutumia dawa ya kuzuia kama vile aspirin, ili kupunguza hatari ya shinikizo la moyo.

"Sasa tuna ushahidi mkubwa kwamba hizi ni dawa zinazonusuru afya, baada ya ubongo kutoa damu, ikisaidia kuokoa pia hatari zingine, ambayo ni habari njema kwa wagonjwa na madaktari."

Hata hivyo, kuwapo taarifa hiyo, bado inasisitizwa mtu yeyote asichukue hatua ya kutumia dawa, pasipo ushauri wa daktari. BBC.

Habari Kubwa