Atengeneza feni inayofanya kazi saa 19 bila umeme

27Jun 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Atengeneza feni inayofanya kazi saa 19 bila umeme

Ukoma Michael, mwenye umri wa miaka 13, kutoka Nigeria ni mmoja wa wajasiriamali wadogo wa teknolojia bora zaidi duniani.

Ametengeneza feni inayojiendesha kwa kutumia betri itakayozunguka saa hadi 19 bila ya kutumia umeme. Feni hiyo inajengwa kwa maumbo tofauti yenye urefu wa meza ya kawaida ambayo anaiita " Blue Wind Fans,".

Imetengenezwa kwa maumbo na ukubwa tofauti kutoka kwenye urefu wa meza hadi juu au kuanzia chini inasimama yenyewe.
Jinsi inavyofanya kazi

Michael hutengeneza feni yake kwa kutumia aluminia, waya, na hutumia mabango ya kale ya ufungaji. Hii inafanya utengenezaji kufanikiwa kwa bei nafuu sana katika ngazi ya familia za kipato cha chini kumudu kuitumia.

Hata hivyo, muundo wake unatumia teknolojia ya hali ya juu kufanywa na mjasiriamali mdogo kama yeye.

Michael ana mipango zaidi katika siku zijazo kutengeneza kazi bora zaidi tena kwa gharama nafuu zaidi. Anataka hatimaye kutengeneza sehemu ya injini ndege ili kuhakikisha kuwa, azma yake ya kutengeneza ndege inafanikiwa.

Mwelekeo mpya wa Afrika
Michael anawakilisha mwelekeo mpya wa ukuaji wa teknolojia unaoongezeka katika nchi kama Kenya, Nigeria, Uganda na Afrika Kusini ambako shule zinazidi kujitolea kuwahimiza vijana waendelee kufanya uvumbuzi wa kipekee kwa ajili ya kukabili matatizo ya nchi.

Hii ni hatua muhimu ambayo wanafunzi wa nchi mbalimbali hasa za Afrika, wanastahili kuiga kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.

Mafanikio hayo yanafanikiwa kutokana na kuwa na msukumo wa shule husika kwa wanafunzi wake kujiendeleza kwa kufanya ugunduzi wa kile na hiki na mara kwa mara.

Wajasiriamali wadogo wa teknolojia kama Michael ambao hawaziangushi shule zao, mafanikio yao huzitia moyo shule zao kuendelea kutia msukumo kwa wanafunzi wengineo wafuate nyayo zao.

Habari Kubwa