Auawa na simba anaowafuga

15Mar 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Auawa na simba anaowafuga

MWANAMUME mmoja, ameshambuliwa na simba aliyemfuga nyumbani kwake mashariki mwa Jamhuri ya Czech.

Simba aliyemuua mmiliki wake. PICHA: BBC

Michal Prasek, alimiliki simba huyo mwenye miaka tisa na simba jike aliyemfuga kwa ajili ya kuzalisha, hatua inayoarifiwa kuzusha wasiwasi kutoka kwa wakazi jirani.

Baba wae Prasek, aliupata mwili wake ndani ya kizuizi cha simba huyo na kuambia vyombo vya habari, kwamba kilikuwa kimefungwa kwa ndani.

Wanyama hao waliokuwa wanaishi katika vizuizi tofuati, walipigwa risasi na kuuawa na polisi walioitwa katika eneo hilo kufuatilia mkasa huo.

Msemaji wa Polisi, aliwaambia waandishi habari kwamba, ilikuwa muhimu kwa simba hao kuuawa ili kumfikia marehemu.

Prasek, mwenye umri wa miaka 33, alimnunua simba huyo mwaka 2016 na simba jike huyo mwaka jana na aliwaweka wote katika vizuizi alivyovitengeneza katika ua la nyumbani kwake, katika kijiji cha Zdechov.

Awali alikatazwa ruhusa ya kujenga vizuizi hivyo na alitozwa faini kwa kufuga wanyama hao kinyume na sheria.

Lakini, mvutano wake na maofisa wa serikali, ulikwama baada ya kukataa kuruhusu mtu yeyote kuingia kwake.

Ukosefu wa vituo mbadala katika Jamhuri hiyo ya Czech, imemaanisha kwamba haingewezekana wanyama hao kuondolewa kwa lazima.

Prasek aliteka vichwa vya habari vya vyombo mbalimbali mwaka jana, baada ya mwendesha baiskeli kupambana na simba hao wakati Prasek alipokuwa akiwatembeza, huku akiwa amewafunga kwa nyororo.

Baada ya polisi kuingilia kati, tukio hilo lilitazamwa kama ajali ya trafiki.

"Tukio la leo huenda likasaidia hatimaye kutatua tatizo hili la muda mrefu," anasema Meya wa Zdechov, Tomas Kocourek. BBC

Habari Kubwa