BILL GATES: Dawa za kudhibiti vijidudu sugu vyaanza ‘kuchemsha’

05Jan 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
BILL GATES: Dawa za kudhibiti vijidudu sugu vyaanza ‘kuchemsha’

MSAMALIA mwema anaamini kuwa 'zana bora za matibabu zitakuja, lakini hadi sasa dunia inakabiliwa na janga la hatari ya kukabiliana na usugu wa kutibu vimelea ambavyo dawa zinashindwa kukabiliana nazo .

Inadaiwa watu duniani kote, hasa wale walio katika nchi zinazoendelea, wanakabiliwa na mwongo wa hatari kutoka kwa maambukizi mapya ya magonjwa sugu, miili kukosa kinga kikamilifu na dawa za kukabili maambukizi hayo kukosa uwezo huo ameonya , bilionea Bill Gates.

Gates, ambaye amepata bahati ya kupanda ngazi ya mafanikio kiuchumi kupitia mfumo wa kompyuta uitwao Microsoft Windows kabla ya kujitokeza kuwa mmoja wa wa wafadhili wa afya duniani, alisema dawa za kudhibiti vijidudu zilileta mafanikio ya kuridhisha kabla ya kujitokeza vijidudu ambavyo ni sugu kwa dawa.

HATUA ZA KUCHUKULIWA 2017
Mtaalamu, Steven Heim: "Ninakunja vidole yangu wakati wote, kwamba baadhi ya majanga kama maambukizi ya homa kali hayatakuja katika kipindi cha miaka 10 ijayo," Gates alizungumza katika program maalumu ya Radio 4 akiwa mgeni mwalikwa , program iliyohaririwa na Ofisa Mkuu wa Matibabu kwa Uingereza- Dame Sally Davies.

"Ninadhani tutakuwa na zana bora zaidi za matibabu, majibu bora zaidi, lakini sasa tuna mazingira magumu kama kuna kitu kitasambaa kwa kasi sana kama vile homa ambayo ni mbaya kabisa - litakuwa janga na mbinu mpya lazima zituruhusu ili kupunguza kiwango cha hatari kubwa inayoweza kutukabili. "

Gates alisema, ni muhimu kwa nchi tajiri kuchukua hatua ili kusaidia nchi zinazoendelea kupambana na ugonjwa huo, kwa sababu mbili kwanza za kibinadamu na pili, kwa ajili ya usalama wa afya zetu wenyewe.

Licha ya kwamba makosa yalifanywa, upinzani wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wakati wa mgogoro wa Ebola katika Afrika magharibi haukuwa wa haki, alisema, kwa sababu wahusika hawakuwa wamefadhiliwa au kuwezeshwa wataalamu wa afya ili kufanya mambo yote ambayo waangalizi walitaka yafanyike .

Ushirikiano wa kimataifa ulichangia kutokomeza ndui, na ilikuwa katika hatihati ya kutokomeza polio, aliongeza.

"Ushirikiano tuliouona, nadhani, unatakiwa kuimarishwa," alisema Gates. "Ni njia pekee matatizo ya kimataifa kama maambukizi ya magonjwa sugu yanaweza kutatuliwa na hivyo [kwa] watu wote wenye mitazamo hasi kuhusu WHO, ujumbe wa kuuchukua mbali kutokana na aina hiyo hiyo ya juhudi za kimataifa kwa ushirika wa wadau, umepotea na matumizi ya fedha si mazuri , badala yake kuna haja ya kupanua uwezo wao.

Sisi kwa kweli tunahitaji kujitolea wenyewe kwa ushirikiano huu wa kimataifa. "

Mwezi Septemba, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, alionya kuwa, upinzani kuhusu dawa za kudhibiti vijidudu "ni tishio la kimsingi " kwa kuhatarisha afya ya kimataifa ambalo haliwezekani.

Inakadiriwa kuwa, zaidi ya watu 700,000 hufa kila mwaka kutokana na maambukizo sugu, ingawa takwimu zinaweza kuwa juu zaidi kwa sababu hakuna mfumo wa kimataifa wa kufuatilia takwimu.

Pia kumekuwepo na matatizo katika kufuatilia uwepo wa vifo vingi, hata katika maeneo ambayo kuna ufuatiliaji , kama vile Marekani, ambayo maelfu ya vifo hivyo huchangiwa na bakteria sugu , kwa mujibu wa uchunguzi wa shirika la habari la Reuters .

Taarifa ya Kituo cha Ulaya cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa(.The European Centre for Disease Prevention )mwezi Novemba kwamba, magonjwa sugu yamekuwa yakishindwa kukabiliwa na dawa za kudhibiti vijidudu zijulikanazo –last line antibiotics- ambayo huwekwa katika kundi la dawa za akiba ,ambazo hutumika baada ya dawa nyinginezo kushindikana kutokana na vimelea kuthibitika kuwa sugu kwa dawa nyinginezo viliongezeka katika bara la Afrika Bila wao, baadhi ya magonjwa yangeweza kuwa hayatibiki na aina fulani ya upasuaji mkubwa utakuwa hatari kwao .

Davies alisema, huduma ya afya ya Uingereza ni pamoja na kushughulikia maambukizi , ingawa bado itachukua muda mrefu kama miezi sita "kuzalisha chanjo ya kutosha kuanza kutumiwa na watu". Alikuwa chini ya matumaini kuhusu jinsi gani jamii nyingine ya Uingereza itakuwa endapo magonjwa ya mlipuko yatatokea.

"Siyo tu NHS," alisema. "Ni jinsi gani mfumo wetu wa huduma za kijamii unaweza kukabiliana na watu ambao si wagonjwa wa kutosha kuwa hospitali, lakini wanahitaji msaada wa ziada? Ni jinsi gani uchumi wetu utaweza kukabiliana kama sehemu kubwa ni wagonjwa sana kuweza kufanya kazi? Wakati tunatoa sera tu- na kuagiza kwa ajili ya utoaji wa chakula, petroli, chochote.

"Na kama unadhani kuhusu masuala ambayo yanaweza kutokea hapa kama kujirudia kwa mafua mwaka 1918 , je itakuwa kama ilivyo katika nchi za kati na zenye kipato cha chini ambao hawana mifumo wa afya wa kuangalia wagonjwa? "

Imetafsiriwa kutoka jarida la Market Finder.

Habari Kubwa