Binadamu wa kale Israel walivyohifadhi nyama pangoni

12Nov 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salam
Nipashe
Binadamu wa kale Israel walivyohifadhi nyama pangoni

WANASAYANSI nchini Israel, wanasema kuwa wamepata ushahidi kwamba binadamu wa kale walihifadhi nyama kwa lengo la kula siku zijazo.

Katika uchunguzi wao wanasayasi walipata alama katika ngozi ya mifupa iliyohifadhiwa.PICHA: MTANDAO

Ushahidi huo umebainisha kuwa watu walioishi miaka kati ya 200,000 na 420,000 iliyopita, walikuwa na uwezo wa kung'amua mahitaji yao ya baadaye, wanasema. Watafiti walichunguza mifupa iliyopatikana katika pango la Qesem karibu na mji wa Tel Aviv.

Waligundua alama katika mifupa iliyokatwa, ikiashiria ni mbinu ya kuhifadhi chakula kisiharibike ili kiweze kuliwa baadaye.

Watafiti wanasema alama hizo ziliwekwa kwasababu binadamu wa kale hawakuwa na uwezo wa kutoa ngozi iliyokauka kwenye mfupa uliohifadhiwa kwa muda mrefu. Alama hizo zilionekana kwa asilimia 78 ya zaidi ya mifupa 80,000 ya wanyama waliochunguza.

“Mafuta yanayopatikana katika mfupa huwa chanzo muhimu cha lishe bora…Kufikia sasa, ushahidi umeashiria utumiaji wa mara moja wa korongo kufuatia uchunguzi uliofanyiwa mifupa hiyo baada ya kuondolewa kwa tishu laini,” anasema Ran Barkai kutoka Chuo Kikuu cha Tel Aviv nchini Israel.

Binadamu wa kale walikuwa wakiwinda kulungu la mwendo, walihifadhi miguu na fuvu la kichwa cha wanyama hao pangoni na kisha kuondoa mabaki ya mnyama katika eneo alipouliwa, anasema Profesa Jordi Rosell wa Chuo Kikuu cha Rovira Virgili nchini Uhispania.

Watafiti walithibitisha kuwa hali katika pango hilo iliruhusu mafuta kwenye mifupa iliyohifadhiwa kuwa lishe kwa hadi wiki tisa, baada ya mnyama huyo kuuawa.

BBC

Habari Kubwa