Corona inavyokoleza ‘mipasho’ kati ya Wamarekani na China

25Mar 2020
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Corona inavyokoleza ‘mipasho’ kati ya Wamarekani na China

NI wazi kuwa sasa dunia iko katika wakati mgumu ina uhusiano kati ya Marekani na China haujatengamaa.

Trump kushoto na hasimu wake Rais wa China, Xi Jinping. PICHA:BBC

Rais Donald Trump wa Marekani amekuwa akitoa matamshi ya mara kwa mara ya kejili kuwa virusi vya corona ni "virusi vya China"-‘China virus’.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo naye anaviita "virusi vya Wuhan", kwenye jimbo la Wuhan ndiko chimbuko la COVD 19 , jambo ambalo pia limeikera sana China.

Rais na waziri wa mambo ya nje wote wanailaumu China kwa kushindwa kukabiliana na mlipuko huu, lakini msemaji wa China amekanusha madai yao na kusema kuwa waliokuwa China walishuhudia kuwa ilikuwa wazi katika tatizo hilo kuanzia mwanzo kabisa.

Kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii kuna tetesi zinazodai kuwa ugonjwa huu umesababishwa na mpango wa wanajeshi wa Marekani.

Wakati wanasayansi wanapinga madai hayo na kusema kuwa ugonjwa huo virusi vyake ni vya asili na hakuna aliyevitengeneza, kila mmoja anamini lake.

Lakini, hii si vita ya maneno peke yake, kuna mapambano zaidi yanayoendelea.

Mapema mwezi huu, wakati Marekani ilipotangaza kufunga mipaka yake yote kwa wasafiri wengi wa mataifa ya bara la Ulaya, Italia ikiwemo serikali ya China imetangaza kutuma vifaa tiba Italia, taifa ambalo linaongoza kwa maambuizi mengi ya virusi vya corona au COVID 19.

China imetuma msaada wa kukabiliana na corona kwa nchi za Iran na Serbia pia. Ni wakati ambao tunaona ishara kubwa, China inasema.

Hii ni ishara ya mapambano ya taarifa kwa kile ambacho kiko nyuma ya pazia, huku China ikiwa inapata unafuu katika janga hili lakini janga limegeuka kuwa la dunia.

China inaongeza kuwa kiukweli, mapambano haya kwa Marekani, ni wakati ambao inabidi washushe mikono yao chini.

Taarifa zinasema msaada wa vifaa tiba wa ndege ndogo ya vita ya Marekani nchini Italia ni mgumu kuwa msaada wa kutosha.

Huu ni wakati mgumu ambao mamlaka na mfumo wa kisiasa katika mataifa yote yanakabiliana nao na hawajawahi kukutana na hali kama hii hapo kabla.

Viongozi watakuwa katika hali ngumu ya kiuchumi na kwamba viongozi ambao wako madarakani watalaumiwa kwa kushindwa kuabiliana na tatizo hili , ufanisi wao katika uongozi utahukumiwa na watu kwa kushindwa kukomboa nchi zao kutoka katika ugonjwa huu mpya.

Ugonjwa wa corona umekuja wakati ambao Marekani na China walikuwa tayari katika uhusiano ambao si mzuri.

BBC

Habari Kubwa