Dk. FRANCIS ROMAN: Mradi wa maboresho hospitali za rufaa umetupaisha

07Apr 2016
Frank Monyo
Dar
Nipashe
Dk. FRANCIS ROMAN: Mradi wa maboresho hospitali za rufaa umetupaisha
  • Hospitali teule ya Kibosho ni tegemeo kwa wagonjwa wa meno baada ya kutekelezwa mradi wa S5 Kaizen wenye lengo la kuboresha huduma katika sehemu za kazi unaoendeshwa na Shirika la JICA

AFYA ya kinywa na meno imekuwa changamoto kubwa kwa watu wazima na watoto, kutokana na wengi kulalamika kinywa chao kinatoa harufu mbaya, fizi kutoa damu,menio yao kutoboka na maumivu makali.

Mtaalamu bingwa wa kinywa, Dk. Francis Roman (kushoto), akimhudumia mgojwa wake katika Hospitali Teule ya Kibosho.

Mtaalamu bingwa wa tiba ya kinya na meno kutoka Hospitali Teule ya Kibosho iliyopo mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Francis Roman, anakiri kuwepo ongezeko kubwa la tatizo la afya ya kinywa na wagonjwa wa meno tofauti na miaka iliyopita kwa rika zote.

Anasema kuwa, katika hospitali ya Kibosho wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutoa kulikabili tatizo hilo, ikizingatiwa ni hospitali pekee katika Kanda ya Kaskazini inayotibu na kutoa ushauri wa afya ya kinywa na meno kwa kiwango hicho cha utaalamu wa juu.

Anajigamba kinachofanya hospitali hiyo kuwa tofauti na nyingine, ni kutokana na kuwa na vifaa vya kisasa na kuwa na huduma ya X-ray za meno pekee kwa hospitali za mkoa wa Kilimanjaro, sambamba na wataalamu waliobobea katika idara hiyo.

Dk. Roman anasema kutokana na hospitali hiyo kubobea katika kutoa matibabu hayo, wamekuwa wakipokea wagonjwa kutoka nje ya mkoa kwa ajili ya matibabu, wanaofikia wastani wa asilimia kati ya 60 na 65.

Anafafanua kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ilyopita, maboresho hayo yameendana na ongezeko la kubwa la wagonjwa wa meno.

Wagonjwa hao wanatoka hasa kutoka maeneo ya Moshi, Same, Mwanga mkoani Kilimanjaro, Arusha na Dar-es-Salaam.
Mtaalamu huyo anasema mwaka jana walitibu wagonjwa 3,220 ikiwa ni ziada ya wagonjwa 220 ya mwaka 2014, kwea maana ya waginjwa 3000. Mwaka 2013 walitibiwa wagonjwa 1657.

“Hapa hospitalini kwetu kuna daktari Bingwa wa meno mmoja ambaye ni mimi na madaktari wawili, vyumba vinne vya matibabu huku kila kimoja kikiwa na msaidizi mmoja na mashine za kisasa ikiwamo X- ray,”anasema.

Anasema tatizo la afya ya kinywa na meno linakuwa kwa kasi, kwani ilizoeleka watu wenye umri mkubwa hasa wazee ndio walikuwa wakisumbuliwa na maradhi hayo na kusababisha mdomo kutoa harufu kali.

Anasisitiza kwamba hivi sasa matatizo ya meno kwa watoto na vijana wenye umri wa kati ya miaka 13 hadi 28, yameongezeka na kuwa kero inayowasababishia vijana wakose raha kwa meno yao kuioza na kutoa harufu mbaya.

SIRI YA MABORESHO
Dk. Roman anasema mafanikio katika eneo lake hilo la taaluma mna kazi, yanatokana na Mradi wa Uboreshaji Mazingira Sehemu ya Kazi katika Hospitali za Rufaa za Mikoa na Wilaya unaoendeshwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) unaojulikana kwa jina la S5-Kaizen.

Anasema mpango wa mradi huo ulianza mwaka 2011, katika hospitali hiyo kulingana na mpango wa ubora wa Wizara ya Afya huku ikishirikiana JICA.

“JICA ndiyo iliyopewa jukumu la kusimamia mpango wa ubora katika hospitali, kuanzia za Rufaa za mikoa na wilaya, kwa kutoa mafunzo na kusimamia utekelezaji wake, ili kuongeza ufanisi wa kazi na kutoa huduma bora,” anasema.

Daktari huyo anafafanua kuwa utekelezaji wa mpango huo ulianza hospitali hapo, baada ya Kamati ya Uendeshaji wa Hospitali kupatiwa mafunzo na baadae kuunda timu ya usimamizi wa ubora iitwayo QIT na ile ya kusimamia ubora wa kazi - WIT.

Ananafanua maana ya S5 Kaizen, ni falsafa ya Kijapan inayomaanisha kusimamia mpango na mtiririko wa kazi ofisini au kwenye taasisi, kwa lengo la kuboresha ufanisi, kwa kuondoa uchafu, kuboresha mtiririko na kupunguza michakato isiyo ya lazima.

Anafafanua kuwa maana ya dhana ya S5 Kaizen ni neno la Kijapani lenye maana kuwa ya kwanza inasimama kwa neno Seti, (kupanga) ya pili Sasambua (kupangua) ya tatu Safisha, ya nne Sanifisha na ya tano Shikilia.

Dk. Roman anasema kabla ya mradi huo kuanza, walishindwa kutoa huduma bora kutokana na kukosa mpangilio sahihi wa vifaa vya kazi, iliyosababisha kutumia muda mrefu kutafuta kumbukumbu za wateja.

“Mradi huu wa S5 Kaizen, umetusaidia kuweza kupanga dawa kwa utaratibu, kumbukumbu na hata alama zinazoonyesha huduma husika na kufanya mgonjwa anapofika anahudumiwa kwa haraka tofauti na awali,” anasema Dk. Roman.
Anasema dhana ya kwanza inaitwa Seti; Hiyo, inamaanisha kutenganisha vitu vinavyohitajika na visivyohitajika maeneo ya kazi ili kubaki na vitu vinavyohitajika.

“Ukiwa umeseti na kupangilia vifaa tiba vizuri utakuwezesha kufanya matibabu bila usumbufu au kupoteza muda, kwani vitu vinakuwa katika mpangilio mzuri na kuelekeza kwa majina au alama, ili kuonyesha mahali stahili pa kutunzia vitu hivyo,” anasema.

Kwa mujibu wa daktari huyo, Seti imefanikiwa kupangwa kwa vifaa tiba katika idara ya meno vinavyotumika kufanyia uchunguzi, upasuaji, dawa na ratiba za upasuaji, pia kliniki za wagonjwa wa meno.

Dk. Roman anataja dhana ya pili - Safisha, ikimaanisha kusafisha na kukagua maeneo ya kazi na vifaa; kuvitunza katika hali nzuri ya usafi.

Anasema dhana hiyo imesaidia kuweka mazingira ya hospitali pamoja na chumba cha upasuaji katika hali ya usafi na kuondokana na wagonjwa kupata magonjwa ya kuambukiza.

Dhana ya tatu kwa mujibu wa Dk. Roman ni Sanifisha; Hiyo dhana yake ni kuweka vielelezo na kanuni za kusanifisha mahali pa kazi, kwa kutumia mfumo unaoaminika, ili kurahisisha utendaji wa kazi kwa wakati.

Anataja dhana ya nne ni Sasambua; jukumu lake kwa mujibu wa mtaalamu huyo bingwe ni kupanga na kuondoa vitendea kazi vilivyopitwa na wakati, huku dhana ya tano anataja kwa jina la Shikilia.

MAFANIKIO YA MRADI
Kutokana na hatua hizo zilizochukuliwa na mamlaka za kigeni ni kwamba kuna mafanikio baada ya mradi huo kuanza kazi, ikihusu maeneo ya usalama na urahisi wa kazi za watumishi wachache.

Anataja lingine ni kuwepo ubora wa huduma unaomrahisishia mgonjwa apunguze mlolongo wa kupatiwa huduma.

Dk. Roman anafafanua: “Mradi huu wa ‘S5 Kaizen’ haujanufaisha tu kwa upande wa matibabu, bali hata kwa upande wa mazingira ya kuzunguka hospitali yetu, tumetumia mbinu za mradi huu kuboresha na kumfanya mgonjwa ayafurahie.”
Anaongeza kuwa mradi umewezesha kuwapo mipango ya kutoaa elimu ya kinywa na meno, kuziba meno, matibabu ya mzizi wa jino, kuyang’arisha na kusafisha meno, kuweka meno bandia, kung’oa na kufanya upasuaji.

Mtaaalmu huyo anasema kupitia mradi huo, wanaendesha huduma za nje katika zahanati na shule zilizo karibu, wanafika hospitalini kupewa elimu ya kinywa, kuchunguzwa na kadhalika.

MARADHI YA FIZI
NA DALILI ZAKE
Dk. Roman anaingia kwa undani kuhusu fani yake akianza na tahadhari ya umuhimu wa kupigaji mswaki na kutunza meno, kuwa ni jambo muhimu na endapo mtu hatapiga mswaki ipasavyo, pamoja na kutumia nyuzi kusafisha katikati ya meno, anaweza kupata maradhi ya fizi na kuishia meno kuoza.

“Maradhi ya fizi yanasababishwa na utando unaokaa kwenye meno, unaotengenezwa na bakteria, ute na chembechembe nyinginezo ambazo zinazoganda kwenye meno,” anasema Dk. Roman.

Anaeleza maradhi ya fizi katika awamu ya awamu ya kwanza kuwa yanaitwa ‘Gingivitis’ ambayo fizi huwa nyekundu, inavimba na kutokwa damu kwa urahisi.

Mtaalamu huyo anafafanua kwamba iwapo hali hiyo itagundulika mapema, inaweza kutatuliwa kwa kupiga mswaki vizuri na kutumia nyuzi kusafisha katikati ya meno.

Anaieleza awamu ya pili ya ugonjwa wa fizi kitaalamu kwa jina la ‘Periodontitis.’ Ni uvimbe unaotokea kuzunguka jino na ni awamu yenye madhara zaidi ya ugonjwa wa fizi, kwani bakteria wanadhuru utando ulioshikilia jino.

Anasema hali hiyo inasababisha fizi ziachane na jino na kusababisha uharibifu wa mfupa ulioliwa kuzunguka jino kuanza kuonekana.

KINGA YA KUHARIBIKA MENO
Madaktari wa meno wanapendekeza, ni vyema meo yanachunguzwa ama mara moja au mbili kwa mwaka, kutegemea na hali halisi ya meno ya mtu.

Katika uchunguzi, daktari atapiga picha za vipimo vya X-ray na kuchunguza meno ya mgonjwa kwa uangalifu kama yameoza.

Anasema, iwapo atatumia dawa za ganzi na mashine ya kutoboa na kuziba mashimo yoyote bila kumuumiza mhusika.
Dk. Roman anasema kuwa, kwa watoto baadhi ya madaktari wanadhani meno yanaanza kuota tena iwapo kuwa na nyufa, huku vijanahaio wadogo wakipata ugumu wa kupigia mswaki.

Kwa watu wazima, madaktari wa meno huhangaika sana kuzuia ugonjwa wa fizi.

Anasema watu wengi hawasugui baadhi ya sehemu zaa meno yao kila mara wanapopiga mswaki, hivyo madaktari wakati mwingine hutoa malekezo na somo la namna ya kupiga mswaki.

Habari Kubwa