DRC mpya katika umasikini mkuu

11Jan 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
DRC mpya katika umasikini mkuu

JANA usiku wa manane, Jamhuri ya Kidemokarsi ya Congo (DCR), ilipata Rais mpya, Felix Tshekedi, kuchukua nafasi ya Joseph Kabila, aliyeingia madarakani kwa kurithi viatu vya baba yake, aliyedumu muda mfupi sana madarakani.

Migodi ya dhahabu, moja ya utajiri wa DRC. PICHA: MTANDAO.

Wachambuzi wa siasa tangu jana wanautafsiri kuwa uchaguzi wa kwanza huru, kwa nchi ya DRC tangu uhuru wake miongo mitano iliyopita.

Kimsingi, ambayo imepitia majina mengi ya Congo na Zaire, sasa DRC, ni taifa kubwa na la kupendeza, ambalo demokrasia na uchumi wake unaelezwa umekwamishwa na kinachodaiwa historia ya uporaji, unyonyaji, utawala mbaya na ufisadi.

Tangu kuondolewa madarakani kwa Rais Mobutu Sese Seko mwaka 1997, taifa hilo bado limeendelea kugubikwa na vita na misukosuko ya kisiasa, ambayo kila wakati hutishia kugeuka na kuwa vita. Mamilioni ya watu wamelazimika kuyakimbia makazi yao kila vita vinapozuka.

Makundi ya waasi wa kivita na watu wenye ushawishi wamekuwa wakuitumia tofauti hizo kijifaidisha kikabila kujifaidisha kiuchumi.

Taifa hilo ni maskini, Umoja wa Mataifa ukisema takriban watu 13 milioni kati ya raia wake milioni 85, wanahitaji usaidizi wa ama aina moja au nyingine, kwani wako katika ufukara uliokithiri.

Ni taifa lenye vijana wengi wachapa kazi na theluthi mbili ya raia wake, wako katika umri chini ya miaka 25. Sasa, wana matumaini na ndoto kuu na wanasubiri fursa kujiimarisha na kulikuza taifa lao.

Rais wa sasa, Joseph Kabila, amekubali kuondoka madarakani.

Madini hayo yanayotolewa kutoka kwenye mawe yenye rangi ya kijani iliyochanganyikana na bluu, ni muhimu sana katika utengenezaji wa betri. Umuhimu wake umezidi zaidi katika kipindi kilichopo, ikizingatiwa yanayotumia umeme yameanza kutengenezwa.

Awali ilikuwa inapatikana kama bidhaa ya kawaida, lakini sasa hitaji lake limeongezeka na bei yake imepanda sana katika soko la kimataifa.

Ni bidhaa inayohitajika sana inayofanya machimbo haramu madogo ya madini yanachipuka, kila sehemu. Wanawake na watoto ni miongoni mwa wanaofanyishwa kazi katika migodi hiyo chini ya mazingira hatari.

USAFIRI WAKE

Miundo mbinu nchini DR Congo imo katika hali duni - si katika kasri la Mobutu na mji wake wa kuzaliwa pekee, barabara zimo katika hali mbovu maeneo mengi.

Katika taifa hili la ukubwa sawa na wa Ulaya Magharibi, ni vigumu sana kusafiri mbali.

Njia kuu pekee ya kusafiri mbali nchini humo ni Mto Congo, hivi sasa haitumiki kwa usafiri kama zamani.

Inawezekana kusafiri kwenye mto huo kutoka Kinshasa hadi Kisangani umbali wa kilomita 1,600 na ndiyo njia kuu ya kuwasafirisha watu na bidhaa nchini humo.

Ni ukanda ambao mtoni na kando yake raha yake, ikiwemo kuisafiria, pia ni mahali watu wanafanya kazi zao, kuishi na biashara.

Kwa mujibu wa taarifa za mtandao.

Habari Kubwa