IJUE KAZI YA UTT AMIS;Mkono wa Wizara ya Fedha unaofungua milango,

13May 2022
Frank Monyo
DAR ES SALAAM
Nipashe
IJUE KAZI YA UTT AMIS;Mkono wa Wizara ya Fedha unaofungua milango,
  • Dawa inayotibu magumu ya uwekezaji kwa wote 
  • Darasa kamili; fursa umri wowote;  ‘wanaodunduliza’

KUTOKANA na hali ya uchumi wa Dunia, kuna kundi kubwa la watu wanaojihusisha na biashara au ujasiriamali, wakilenga kujikimu na kuongeza kipato, lakini wako njia panda wafanye nini.

Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu akipewa maelekezo kutoka kwa Ofisa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS, Dorice Mlenge, jinsi mifuko ya uwekezaji wa pamoja inavyowanufaisha machinga wakati wa maonyesho ya wamachinga yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. PICHA: MPIGA PICHA WETU

Wapo wengi wamejiunga na biashara ilhali hawana elimu sahihi ya fedha au namna ya kukabili changamoto katika uwekezaji.Ofisa Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano wa asasi ya UTT AMIS, Rahim Mwanga, anasema mifuko ya uwekezaji ni njia mojawapo sahihi ya kupunguza hatari au changamoto za uwekezaji.Mwanga anaeleza: "Mwekezaji yeyote anahitaji njia sahihi za kupunguza hatari za uwekezaji, ili kuendelea kutunza mtaji na kupata faida za ushindani, anahitaji utaalumu, gawio, uwazi, urahisi wa kuweka na kutoa fedha zake na gharama nafuu za uendeshaji, vyote vinaweza kupatikana kwenye mifuko yetu ya uwekezaji wa pamoja."Taasisi ya UTT AMIS ni ya kiserikali na inasimamiwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa zaidi ya miaka 17 sasa, ikitoa fursa Watanzania kuwekeza katika mifuko yake ambayo ni; Mfuko wa Umoja, Mfuko wa Watoto, Hatifungani, Jikimu, Wekeza Maisha na Mfuko wa Ukwasi ili kutunza thamani ya fedha, kukuza mitaji yao na kupata gawio.Mwishoni mwa mwaka jana, UTT AMIS ilifanya Mikutano Mikuu ya Mwaka ya Mifuko hiyo ya Uwekezaji, huku ikijivunia mafanikio makubwa pamoja na kuwepo changamoto ya janga la Uviko-19.Mkurugenzi Mtendaji wa UTT AMIS, Simion Migangala, akatangaza mafanikio hayo kwa wawekezaji wa mifuko yote imefanya vizuri, kwa kuainisha: Mfuko wa Umoja thamani ya kipande imeongezeka kwa Sh. 104.0 hadi Sh. 740.0 sawa na faida ya asilimia 16.6 kwa mwaka ulioishia Juni 2021.Anasema Mfuko wa Umoja ni wa kwanza kuanzishwa mwaka 2005 na umeendelea kufanya vizuri kwa miaka 16 mfululizo. Anaufafanua uko wazi na unawalenga wawekezaji wenye lengo la muda mrefu na kati.Kwa sasa, UTT AMIS ina jumla ya mifuko sita ambayo ni: Umoja, Watoto, Wekeza Maisha, Kujikimu, Ukwasi na Hati Fungani.INAFANYAJE KAZI?Ofisa Masoko – Mwanga, anaielezea Nipashe namna mifuko ya UTT AMIS inavyofanya kazi huku ikiacha faida lukuki kwa mwekezaji.

Kwanza anasema, UTT AMIS imepewa leseni kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) kukusanya amana kutoka kwa wawekezaji na kuziwekeza.“Tukishapata hizo fedha tunaenda kuwekeza katika masoko ya fedha na mitaji kulingana na waraka wa toleo la mfuko. Faida inayopatikana inarejeshwa na kugawanywa kwa wawekezaji na sehemu ya uwekezaji wao katika mfuko ndio inafahamika kama kipande,” anafafanua Mwanga.Mwanga anasema masoko ya mitaji, ni fedha inayohusisha dhamana za uwekezaji zaidi ya mwaka mmoja. Anafafanua: “Mfano kuna kuwekeza kwenye Hisa ambazo zimeorodheshwa na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), pia kuna kuwekeza kwenye hati fungani za serikali za muda mrefu na hati fungani za kampuni.”

FAIDA YA KUWEKEZA

Mwanga anasema, faida ya uwekezaji inajumuisha nafasi ya kupata faida shindani sokoni, pia hatari za uwekezaji zikipunguzwa kwa kufanya uwekezaji mseto“Mifuko ya uwekezaji inawezesha wawekezaji wadogo kupata fursa za kuwekeza kwenye masoko ya fedha na mitaji kwa viwango vidogo vya fedha tena mara kwa mara.“Wawekezaji, pia wanapata fursa ya kuwekeza kwenye dhamana, ambazo katika hali fulani mwekezaji mmoja mmoja inakuwa ni ngumu au ghali kuweza kupata dhamana hizo,” anasema.“Kampuni ya UTT AMIS, imekuwa ikitoa elimu ya fedha mara kwa mara kwa makundi tofauti juu ya faida na jinsi ya kuwekeza katika mifuko yao, kwa malengo ya muda mfupi hadi mrefu." anasema MwangaMFUKO WA UMOJAMwanga anaeleza, Mfuko wa Umoja uko wazi na wenye uwiano sawa wa uwekezaji, akiufanya kuwa bora na wenye uwekezaji wa kiwango cha kati.

Pia, ni mfuko unaowekeza kiwango kisichozidi asilimia 50 ya fedha zake kwenye hisa zilizoorodheshwa DSE na asilimia 50 nyingine zinawekezwa kwenye masoko mengine ya fedha na mitaji yenye sifa tofauti.Sera ya uwekezaji kwa upande mmoja, ni mpango uliowekwa na mfuko kutawanya rasilimali zake. Pia, ni mpango mkakati na kinga, endapo eneo moja la uwekezaji linafanya vibaya.

Aidha, anaueleza ni uwekezaji kwenye hisa ulio kwa kiwango cha chini, ikilinganishwa na eneo lenye mapato ya kudumu (fixed Income).Mwanga anasema, thamani ya kipande kwa sasa imeongezeka kwa Sh. 104.0 na kufikia Sh. 740.0 kwa kila kipande, sawa na faida ya asilimia 16.6 kwa mwaka ulioishia Juni 2021.Hapo anafafanua kuwa Mfuko wa Umoja ni mfuko wa kwanza kuanzishwa na UTT AMIS mwaka 2005 na umeendelea kufanya vizuri kwa muda wa miaka 16 mfululizo ambapo mfuko huo ni wa wazi ambao unalenga wawekezaji wenye lengo la muda mrefu na wa kati.MFUKO WA UKWASIAnasema, madhumuni ya mfuko huo ni mpango unaotoa njia nyingine ya uwekezaji kwa wawekezaji, wanaotaka kuweka fedha kwa kipindi cha muda mfupi na mrefu. Hatari na athari kidogo katika uwekezaji na ukwasi wa hali ya juu, ndio dhumuni hasa la mfuko huu.Anaieleza Sera ya Uwekezaji kuwa ni kiwango cha chini cha uwekezaji katika masoko ya fedha, itakuwa asilimia 50 na fedha inayobaki itawekezwa katika Dhamana za Serikali. Huo ni mfuko usiowekeza kwenye hisa."Chaguo la mpango wa Uwekezaji wa Mfuko huu; unatoa fursa ya kukuza mtaji. Pia mwekezaji anaweza kutoa fedha zake wakati wowote bila gharama yoyote,” anafafanua.Nani anaruhusiwa kuwekeza?  Mfuko uko wazi kwa Mtanzania aliye ndani au nje ya nchi, ikihusisha mtu binafsi (ikijumuisha watoto), asasi kama mifuko ya pensheni, benki, taasisi za serikali, vyombo vya ulinzi na usalama, asasi zisizo za kiserikali na mashirika mengineyo.

Anaeleza Mfuko wa Ukwasi, umeongezeka ukubwa kwa Sh. bilioni 103.1 sawa na asilimia 91.4; ikimaanisha kutoka Sh. bilioni 112.8 Juni, 2020 hadi shilingi bilioni 215.9 Juni 30,2021.Mwanga anaongeza, pia katika kipindi hichohicho thamani ya kipande iliongezeka kwa shilingi 37.5 sawa na faida ya asilimia 15.3 kwa mwaka."Faida ya Mfuko wa Ukwasi kwa kipindi cha mwaka mmoja ni asilimia 15.3 ikilinganishwa na faida ya asilimia 15.1 ulionakiliwa mwaka uliopita 2020. Faida ya asilimia 15.3 ni tafsiri ya ongezeko kwenye mtaji wa mwekezaji aliyewekeza kwa mwaka mmoja," anasema MigangalaMFUKO WA WATOTOMwanga anaufafanua kuwa,  mfuko huo ni mpango ulio wazi kwa watoto unaokusudia kukuza mtaji kwa muda mrefu kupitia uwekezaji wa mseto, kwa kuwekeza kwenye hisa zilizoorodheshwa kwenye soko la hisa na dhamana.Umri wa mtoto wa kujiunga na mfuko, uwekezaji unafanywa kwa mtoto wa umri chini ya miaka 18 na anayeruhusiwa kuwekeza: kwa Watanzania walio ndani na nje ya nchi, pia watu binafsi, kampuni, taasisi, benki na asasi za kiraia, huku uwekezaji ukitakuwa ufanywe kwa manufaa ya mtoto.Anaeleza, kwa kipindi Juni, 2020 hadi Juni 30,2021 thamani ya kipande iliongezeka hadi kufikia Sh. 455.2 kutoka Sh. 380.9 mwaka jana, akisema ukubwa wa mfuko huo ni Sh. bilioni 4.2, ikilinganishwa na Sh. bilioni 3.5  ya Juni 30,2020 ikiwa sawa na ongezeko la Sh. bilioni 0.7 (+20.0%).MFUKO WA JIKIMUMwanga anasema kuwa lengo la Mfuko wa Jikimu ni kukuza na kutoa gawio kutokana na mapato ya ziada kwa vipindi tofauti, pia kumkuzia mwekezaji mtaji.Anasema, mfuko unatoa fursa mbili za uwekezaji, mapato ya robo mwaka, pia mwaka mzima, kwa kuambatanisha na ukuaji wa vipande.Kiwango cha chini cha uwekezaji katika mfuko huo kwa Mpango wa Mapato ya Robo Mwaka, unatajwa ni Sh. milioni 2 na Sh. milioni 1 kwa Mpango wa Gawio kwa Mwaka; pia Sh. 5,000 kwa Mpango wa Ukuaji Mtaji kwa mwaka.“Kiwango cha chini cha uwekezaji wa nyongeza au unaofuata (additional investment) ni Sh.15,000 kwa mpango wowote wa gawio na Sh.5,000 kwa mpango wa ukuaji mtaji kwa mwaka, hakuna ukomo wa kiwango cha kuwekeza,” anafafanua.Anataja faida nyinginezo katika Mfuko wa Jikimu kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2021, ulilipa gawio lenye thamani ya shilingi bilioni 1.2 au sawa na Sh. 12.0 kwa kila kipande.

"Hadi kufikia Juni 30,2021 rasilimali za mfuko zilifika shilingi bilioni 17.9 ikilinganishwa na shilingi bilioni 17.6 mwaka uliopita," anasema na kuongeza kuwa;“Faida ya Mfuko wa Jikimu iliendelea kuimarika na kuongezeka kutoka asilimia 15.6 katika mwaka wa fedha uliopita (2019/2020) hadi asilimia a18.8 katika mwaka wa fedha ulioisha Juni 30,2021.”HATI FUNGANIMwanga anaeleza Mfuko wa Hatifungani kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30,2021 faida ilikuwa asilimia 15.7 ikilinganishwa na asilimia 16.2  mwaka uliotangulia.

"Mfuko wa Hati Fungani umelipa gawio la shilingi 1.0 kila mwezi sawa na shilingi 12.0 kwa muda wa mwaka mmoja," anasemaMFUKO WEKEZA Mwanga anautaja kuwa Mfuko Wekeza Maisha, una zaidi ya miaka 10 sasa, ukiambatanishwa na faida za bima. Mwekezaji katika mfuko huo, ana lengo la kiasi anachotaka kuwekeza katika muda wa miaka 10, kiwango cha chini ni Sh. milioni moja. Ni hiari yake kuwekeza kwa mkupuo au awamu.“Mtu ukichagua kuwekeza kiasi hicho (Sh. milioni moja) kila mwezi atahitajika kuwekeza kiasi cha Sh. 8,340 tu ili kukamilisha mpango wake wa uwekezaji.“Zaidi ya asilimia 99 ya fedha za mwekezaji huwekezwa na chini ya asilimia moja hutumika kugharamia bima,” anasimulia, akitaja aina ya bima hizo ni za maisha, ulemavu wa kudumu na ajali.Mwanga anatoa mfano binafsi, baada ya miaka 10 alifungua kiwanda kidogo cha kutotoa mayai ya kuku na kuuza vifaranga na mayai, akifafanua: “Niliweza kununua mashine (incubator) kwa sasa kipato changu kimeongezeka sana.”Mwanga anakumbusha ukubwa wa mfuko huo kwa sasa umeongezeka kwa Sh. milioni 400  (ziada 28.6%) hadi shilingi bilioni 1.8 kutoka shilingi bilioni 1.4 mwaka 2020.

"Thamani ya kipande kwa muda wa mwaka mmoja ulioishia Juni 30,2021 iliongezeka kwa shilingi 125.8 (25.6%) hadi kufikia shilingi 617.3 kwa kila mwaka." anasema

Habari Kubwa