Kanisa Nigeria lililogeuzwa wodi ya kujifungua lawateka wajawazito

07Apr 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Kanisa Nigeria lililogeuzwa wodi ya kujifungua lawateka wajawazito

KINAMAMA wengi wajawazito hufika kumuona Sista Indoreyin Sambhor, ambaye ni mhudumu wa uzazi, pia Mchungaji wa Kanisa la Nchi ya Ahadi.

Sista Indoreyin Sambhor (aliyesimama), akiwahubiria weajawazimto waliofika kanisani kwake. (PICHA NA MTANDAO).

Hapo anaonekana mwanamama Ransom Linus Martin, ambaye ni mjamzito wa mkazi wa jiji la Calabar, ambako amepanga kujifungua.

Huyo hayuko peke yake. Kuna kundi la wengi waliaomua kufanya mahali hapo kuwa kituo cha kujifungua, mfumo ambao serikali ya Nigeria inaweka dhamira ya kupakomesha.

Mwanamama huyo anayeonekana katika vazi la gauni refu na kofia, anapoulizwa sababu za kutaka kujifungua kanisani badala ya hospitalini ambako kuna huduma rasmi za kliniki, anajibu:

"Wanafunga na kuomba hapa na kama wewe ni mjamzito, unahitaji kwenda katika sehemu ya Mungu ambako watu wanafunga na kuomba kila siku.”

Anaongeza: “Hospitalini hakuna maombi pekee, wanachokupatia ni sindano. Lakini unaposali kanisani unamkaribia Mungu. Katika siku ya kujifungua, Mungu atakusaidia na utajifungua vizuri.”

Mwanamke huyo anafafanua kuwa, imani yake ni kwamba“kanisa ni ulinzi na ndiko kunakopatikana huduma bora za afya.”

Hata hivyo, katika upande wa pili wa hoja hiyo kuna taarifa zisizoridhisha kuwa kinamama wanakufa wakati wanapopata huduma za uzazi mahali hapo.

Hilo linalifanya kanisa hilo liwekwe rasmi katika mtazamo kwamba, mahali hapo si salama kwa ajili ya huduma za kujifungua.

MTAALAMU DK. LINDA AYADE

Dk. Linda Ayade ni mtalamu wa afya na mke wa mmoja wa magavana wa Nigeria. Anasema:"Nina uzoefu kwamba mjamzito anawaishwa hospitali akiwa na hali mbaya na ni vigumu kumsaidia.”

Kutokana na hilo, anasema yuko mstari wa mbele kupinga mwenendo huo wa kanisa na wakati huo huo huo na anawahimiza kinamama kuvitumia vituo vya afya na hospotali kwa ajili ya kujifungua.

Mwanamama huyo ambaye kitaaluma ni daktari, aliamua kufanyia kampeni katika kijiji kimoja kupinga aina hiyo ya huduma za uzazi, akifafanulia kupitia lugha yao ya asilia kwamba:

“Baadhi huwa wanawasilishwa hospitali wakiwa wameshakata roho na inatokea mara nyingi.

“Ninalichukua hili kuwa wajibu wangu kupunguza matukio ya vifo na kujifungua, nikijua nini hasa maana ya mama kufariki na kumuacha mtoto.”

‘KLINIKI’ YA KANISANI

Katika Kanisa la Ahadi ya Mungu, mara zote hutawaliwa na mkusanyiko jumuiko wa kinamama wajawazito wanaomuomba Mungu awafanikishie uzazi salama na kwa wakati sahihi.

Ndani ya ukumbi wa kusali kanisani humo, jirani yake kuna chumba kidogo ambacho kina mazingira machafu na huduma yake ya mwanga ni chemli ya mafuta ya taa.

Katika utetezi wake dhidi ya hoja zinazopingana na kinachofanyika kanisani mwake kuhusu uzazi, Mchungaji Indoreyin anasema ametoka mbali na huduma hiyo tangu akiwa nyumbani kwenye familia alikozaliwa.

"Hii ni kazi niliyopewa na Mungu niifanye. Tangu ujanani nimemsaidia mama yangu kuhudumia wanaojingua. Mungu hataruhusu itokee balaa lolote au jambo baya litokee.

"Ninaomba pamoja na kinamama na wafuasi wangu, kuthibitisha ujuzi wangu, kila mwanamke mjamzito anayekuja kwangu amejifungua salama na aondoka na mtoto wake."

Mahali hapo ndiko anakoonekana mwanamke Mercy Udofia (26) akiwa na mimba ya miezi minane. Naye katika hoja yake, anamuunga mkono mchungaji akisema ni mara yake ya pili kutaka kujifungua, mtoto wa kwanza alijifungua mahali hapo.

"Ukiwa mwana wa Mungu, hupaswi kubweteka tu. Unapaswa kuwa karibu na Mungu, hivyo hata unapokuwa mjamzito na unaopofika wakati wa kujifungua, kila kitu kitakuwa sawa,” anasema mjamzito huyo.

Wakati mama huyo mjamzito akitoa utetezi, tayari kulikuwepo kashfa ya mjamzito kufariki kanisani hapo wakati wa kujifungua watoto mapacha. i

Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu, kifo cha mama huyo kilitokana na matatizo ya uzazi wakati wa kujifungua na watoto waliozaliwa walipona na hivi sasa wako hospitalini mjini Calabar.

Inaelezwa kwa mamlaka za kiserikali zinajipanga kuchukua hatua kuhusiana na tukio hilo.

Mkuu wa Wakala wa Afya ya Msingi, Betta Edu, anasema serikali itasimamisha mara moja shughuli hizo za kujifungua kanisani, ili wajawazito wapiti mamlaka halali.

Anaeleza hisia zake kuwa kuna maelekezo potofu kutoka kanisani dhidi ya huduma za hospitalini, kwamba kinamama wengi wanajifungua kwa opereshehi na kwa sehemu kubwa wanakufa kwa sababu ya kutokwa damu nyingi.

Kiongozi huyo wa afya anasema, kutokana na mazingira hayo, yanawafanya wanawake wazikimbie hospitali na kuelekea kanisani.

Dk. Edu anasema njia nzuri ya kukomesha mwenendo huo ni kufanyika mabadiliko ya sheria.

“Watu wetu ni waumini sana wa dini na baadhi yao wamezama katika mambo ya kimila inayoleta ugumu wa kuwaengua,” anasema na kuongeza:”Tunahitaji kuwaelimisha.”

Habari Kubwa