Kifahamu kijiji kisafi zaidi bara Asia

16Jun 2016
Na Mwandishi Wetu
Meghalaya, India
Nipashe
Kifahamu kijiji kisafi zaidi bara Asia

Kijiji cha Mawlynnong kilichoko nchini India, ndicho kinatajwa kuwa bora kwa usafi barani Asia.

Sifa yake nzuri imemfanya Waziri Mkuu Shri Narendra Modi, aandae programu maalum ya kukisaidia kijiji hicho kupata mfumo bora wa majitaka ambayo haikuea nayo.

Ni kijiji ambacho wakazi wake wanaichukulia kwa umakini suala la usafi kwa jumla.

Katika kijiji hicho kilichoko kwenye mkoa wa Meghalaya na kina jumla ya wakazi 600, kunapatikan kila aina ya uchafu na wakazi wake wanaushambulia ‘kama nyuki’ pindi unapoonekana.

Ni hali tofauti sana kimazingira na vijiji vingine ambavyo vingi fvvimetawaliwa na kinyesi cha ng’ombe na uchafu wa aina nyingine mwingi.

Mwaka 2014, Waziri Mkuu Shri Narendra Modi, alizindua kampeni ya kuwa na India safi na iliyo nadhifu kwa miji yote ya nchi.

Kampeni hiyo inalenga kufikiwa mwaka 2019 katika tarehe ya kuadhimisha tarehe ya kuzaliwa aliyekuwa Waziri Mkuu Mahtma Ghandhi.

Kijijini Mawlynnong, chenyewe kimeshasonga mbali sana, kwani tangu mwaka 2003 kilitangazwa kuwa kijiji safi zaidi barani Asia.

Mwaka jana tena kijiji hicho kilifanikiwa kutwaa suifa ya hadhi hiyo ndani ya India na mwaka huu, program za redio ziliimwagia sifa kijiji hicho kisafi cha India na Bara Asia kwa jumla.

Mtu anapoingia katika mandhari ya kijiji hicho, mara moja atabaini kwamba hakuna hata chembe ya uchafu inayozagaa ndani ya mazingira yake.

Hiyo inaenda mbali hata kwa watoto wanaocheza mitaani, wanaonekana nadhifu maradufu, ikiliganishwa na watoto wengine katika maeneo tofauti ya vijiji, hata mijini.

Wakati kufikia maendeleo hayo nchini India ni mtihani mkubwa, kijijini hapo jambo rahisi kwao na wameshavuka malengo ya kitaifa.

WATOTO NAO HAWASHIKIKI

Kuna swali ambalo limekuwa linaulizwa kulikoni hilo limefanikiwa? Jibu linalotokeza ni kwamba walianzia utotoni.

Hilo linajionyesha kwa mtoto mwenye umri wa miaka 11, ambaye mapema saa 12.30 asubuhi alikutwa na wenzake wakisafisha mazingira ya kijiji, kwa kufagia majani na kuondoa uchafu unaozagaa mitaani.

Baada ya hapo, wanaendelea kutupa taka kutoka kwenye pipa zilizowekwa sehemu mbalimbali, ili kusiwapo uchafu uliosambazwa katika sehemu tofauti.

Uchafu huo una utaratibu maalum wa kufukiwa, ili kuvifanya vitoweke kabisa kwenye mazingira tajwa.

Pia kuna watu waliojitolea kupita mitaani kung’oa majani na mimea mingine inayoota ovyo barabarani na kugeuka kero barabarani.

Mtoto huyo aliyekutwa, aliuzwa juu ya hisia zake kuishi katika kijiji hicho kisafi naye alikiri kwamba ‘anafurahia.’

Pia aliulizwa hatua anayoweza kuchukua iwapo atamkuta mgeni anayewasili kijijini na kutupa taka ovyo, mtoto alijibu: “Sitachukua hatua yoyote bali kuokota uchafu uliotupwa ovyo na kuiweka katika sehemu sahihi.”

Mtoto huyo anafafanua anazidi kwamba, katika maisha yao kijijini Mawlynnong, wana ratoba ya kawaida ya kufanya usafi kila Jumamosi kwa mwanakijiji.

Ni jambo ambalo mtoto huyo anasifu kwamba lina manufaa hata kwa shule yake kuwa safi.

Pia katika ziara ya ki-uanahabari iliyofanywa katika nyumba anakoishi mtoto huyo na wakakutwa mfanyakazi wa nyumbani, mama wa mtoto na bibi yake, kulikuwa na mvuto wa kipekee.

Kila mahali katika nyumba hiyo kuanzia jikoni, sebuleni hadi chumbani kulikuwapo usafi uliotukuka.

USAFI UMETOKEA WAPI?

Mkazi wa kijiji hicho, Shishir Adhikari, anasema tabia inayodhaniwa kujengeka kutokana na kujihami kwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu miaka 130 iliyopita.

Pia inaelezwa, Wamissioanri waliofika kijijini hapo awali ndio walichangia katika kujenga tabia hiyo ya usafi kwa jamii ya wanakijiji.

Lingine la kihistoria alioleleza ni kwamba wakazi husika ni wapenzi wa kuoa mke zaidi ya mmoja na kukifanya kijiji kiwe na wanawake wengi, wanaoelezwa kuwa kundi la wanajamii wanaopenda usafi, kuwashinda wanaume.

“Sisi ni Wakristo kwa zaidi ya miaka 100 iliyopita na usafi ni jambo tuilojinfunza kutoka kwa watangulizi wetu,” anatamka mama wa nyumbani aitwaye Sara Kharrymba.

Anaongeza:“Nahamisha utaalamu huu kutoka kwangu hadi kwa wanangu nao hadi kwa watoto wao.”

Kharrymba anasema suala hilo lilikofikia, usafi ni zaidi ya tabia kwao, bali utamaduni uliojijenga kwa muda mrefu.

Anasema licha ya mwanawe mwenye umri wa miaka sita hawajawahi kutoka nje ya kijiji, tayari anaeleza kufurahishwa na uhalisi wa usafi ulioko katika kila nyumba anayoshuhudia mahali kijijini hapo.

Mwanamke huyo anaongeza kuwa mwanawe anasifu kila nyumba kijijini kuwa na choo kisafi na watoto walioko huko wanatiii utaratibu sahihi wa kutumia choo majumbani kwao.

Habari Kubwa