Kijue kitunguu maji na faida zake kwa afya yako

26Mar 2020
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Kijue kitunguu maji na faida zake kwa afya yako

KITUNGUU maji ni aina ya mboga yenye harufu kali inayochangamsha mwili. Pia, ni kiungo ambacho kina virutubisho katika vyakula na kuvifanya viwe na ladha nzuri.

Bidhaa ya kitunguu, kizima na kilichokatwa. PICHA: MTANDAO.

Nchi mashuhuri na maarufu inayolima kiungo hicho ni Misri na kusambaa zaidi duniani na nchini Tanzania, kinalimwa zaidi katika mikoa kama Morogoro, Iringa, Arusha kwenye rutuba nzuri ya kustawisha kiungo hicho.

Vinaelezwa kitaalamu ni aina ya mboga ya ‘Yungiyungi na inatajwa kuthibitika kisayansi kuwa na manufaa makubwa sana katika afya ya mwanadamu.

Kiungo hicho kimekuwa kikitibu na kuponya maradhi mbalimbali kutokana na kuwa na madini ya salfa ambayo ni nzuri, hasa kwenye ini na husaidia kuponya kansa kwenye utumbo na kinywa, kutokana na kuwa na virutubisho vingi vya vitamini C.

Kitunguu maji kina kazi nyingi mwilini mwa binadamu, inatibu magonjwa ya kikohozi, vidonda vya tumbo na mifupa, ngozi koo, figo, tumbo na mkojo, kufunga hamu ya kula, hutia kiu na hulainisha tumboni.

Pia, ni chanzo cha madini mengi yanayopatikana katika kiungo hicho, ambayo ni umuhimu katika mwili wa binaadamu.
Licha ya umuhimu huo, pia inamarisha afya ya moyo, kuzuia kansa, inakinga mwili dhidi ya vidonda vya tumbo na kuongeza joto la mwili, ikizuia vimelea vya magonjwa mbalimbali katika mwili wa binadamu.

Faida zake katika mwili wa binaadamu ni pamoja na kuupa mwili nishati, kuongeza nguvu, huimarisha misuli ya mwili, kuongeza hamu ya kula, inalainisha tumbo na kuondoa tatizo la kukosa choo.

Pia, faida nyingine ya kitunguu ni kuwa kinatibu pumu, uvimbe wa pafu, saratani, majipu, mvilio wa damu, kufungua choo, kupunguza uzito na chunusi.

Kitunguu maji kinaweza kutengenezewa juisi kwa kukikatakata na kisha kukisaga kwa blenda kwa kuchanganya na maji ya kunywa mara unapojisikia vibaya hasa kwa watu ambao wanasumbuliwa na kifua mara kwa mara.

Pia, unaweza kuchanganya na asali na kunywa nayo ikakusaidia kwa kiasi kikubwa kutibu maumivu ya tumbo na uvimbe mwilini. Maji ya kitunguu kwa mujibu wa wataalamu wa tiba wanasema yanatibu matatizo ya macho.

Juisi yake inaua vijidudu vya kifua kikuu. Kuna tafiti za kisayansi zinazobainisha kuwa na mchango katika kuwa na uwezo wa kuua vijidudu vinavyosababisha maradhi ya kifua-kikuu(baada tu ya mgonjwa kunusa moshi wake)

Uso nao unanawiri pale kitunguu kuchomwa kinapoliwa huufanya uso kuwa mweupe, mn’gavu na unaonawiri.

Kingine, kinasaidia tatizo la kukosa haja kubwa, huku kikipikwa na kuliwa pamoja na samli, kusaidia kuongeza nguvu za kiume.

Upande wa kinamama, kitunguu kikitengenezwa supu pamoja na nyama, huongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake.

Kinasaidia kutibu homa ya manjano na kinavunja mawe tumboni na kutibu tatizo la hedhi kwa wanawake.

Ina msaada kwa wagonjwa wa kisukari, maradhi ya moyo, na kuimarisha mfumo wa mzunguko wa damu mwilini.

Ina sumu vyenye nguvu inayoua kaswende, kisonono.

*Ni kwa mujibu wa taarifa za afya mtandaoni. Jinsi kilimo chake kinavyoendeshwa, fuatilia makala kesho.

Habari Kubwa