Kinamama ‘mashoto’ wana uwezo ziada kunusa

14Nov 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Kinamama ‘mashoto’ wana uwezo ziada kunusa

WANASANYANSI wamebaini cha kipekee katika baiolojia ya mwanadamu na hisia za harufu, kwamba kinamama wanatotumia mkono wa kushoto wana cha ziada katika nguvu ya kunusa.

Mwanamke atumiaye mkono wa kushoto. PICHA: MAKTABA.

Jarida la kisanyasi liitwalo Journal of Neuron, linasema baadhi ya kinamama ambao hata wakikosa nguvu za mishipa fulani katika ubongo, uwezo wao katika kunusa hauna shaka.

Ugunduzi wa watafiti unaenda mbali, kwamba hilo kamwe halijaonekana kwa wanaume, bali kinamama pekee yao.

Baadhi ya viashiria vilivyotumika kupima uwezo wa kunusa ni kinywaji cha kahawa, maua yenye harufu nzuri na nepi ya mtoto iliyochafuliwa, ama kwa mkojo au kinyesi kikubwa.

Namna harufu hiyo inavyosafiri ni kwamba, pua inaponusa, inasafiri hadi katika ubongo ambako kuna mishipa iitwayo ‘olfactory bulbs’ na ikifanyiwa kazi, ujumbe unarudi tena puani, ndio inapopatikana tendo la kunusa.

Kuna watafiti wengine nchini Israel, katika asasi inayoitwa ‘Weizmann Institute of Science’ wamegundua watu kuwa na uwezo wa kawaida kunusa, hata kama mishipa yao ya fahamu inayowawezesha kunusa (katika ubongo) haifanyi kazi.

Mwanazuoni, Profesa Noam Sobel, anaweka maswali kadhaa ili kuweza kuithibitisha hoja hiyo, kwamba kuna tafiti zingine na marejeo ya kitaaluma yanaeleza hayo.

Bado katika mtaazamo wa kitafiti anasema hajaridhishwa kwanini iwe mwenye mkono wa kushoto pekee? Vivyo, ana ufafanuzi wa kitaalamu namna ubongo unavyosaidiana, kwamba inapotokea sehemu moja ikiathirika, nyingine zinasaida na unusaji uwezekane.

Habari Kubwa