Kinamama wakinga sikio, wanena ulivyo ubia bajeti taifa, afya jinsia

17Jun 2021
Yasmine Protace
Dar es Salaam
Nipashe
Kinamama wakinga sikio, wanena ulivyo ubia bajeti taifa, afya jinsia

BAJETI Kuu ya Serikali ya mwaka huu iliyosomwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba,
imewasilishwa wiki iliyopita ikiwa na sura ya mabadiliko yenye maboresho katika baadhi ya sekta.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi, alipozungumza baada ya kuwasilishwa kwa makadirio ya Bajeti ya Kuu ya Serikali, mwaka huu. PICHA: YASMINE PROTACE

Ndani ya bajeti hiyo, wapo baadhi ya wadau kutoka asasi za kiraia kwa kushirikiana na TGNP Mtandao na vikundi vya kijamii kutoka mikoa mbalimbali, sasa wametoa maoni kupitishwa bajeti hiyo ya serikali.

Kimsingi, Bajeti Kuu ya Serikali ni kielelezo cha namna serikali inajipanga kupendekeza mwelekeo wa
katika sekta mbalimbali zitagharamiwa, ili kuleta mabadiliko kitaifa.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi, anasema kuwa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na wadau, asasi za kiraia na vikundi vya kijamii kutoka mikoa mbalimbali, wanahusika.

Katika majumuisho yake akiwa na jicho la kipekee, anafafanua: "Mnamo tarehe 10 Juni mwaka huu, kupitia mjadala wa Bajeti ya Taifa, tulifuatilia kwa pamoja na kuchambua bajeti ya mwaka wa fedha 2020/21 iliyokuwa ikiwasilishwa bungeni na Waziri wa  Fedha na Mipango, Mwigulu Lameck Nchemba."

Anarejea majukumu ya mashirika yanayotetea  haki za wanawake, yamekuwa wakipigania kwa muda mrefu usawa wa kijinsia, hivyo wanaipongeza   serikali kwa kuchukua hatua kutekeleza kilio chao na kusimamia utekelezaji wa sera na mipango ya maendeleo kwa manufaa ya taifa na raia wake.

HAKI JINSIA

Lilian anaongeza kuwa maeneo yaliyoguswa nayo yanajumuisha sekta ya afya na penye maboresho ya ujenzi wa zahanati 1,198 , jengo la ‘Mama na Mtoto’ katika katika Hospitali ya Rufani ya Mwananyamala Dar es Salaam, sasa inafika asilimia 51 kukamilika.

Pia katika mkoa wa Simiyu, anataja hatua hizo zimechangia kupunguza vifo vya kinamama na  watoto na kuna magumu katika upatikanaji huduma za uzazi salama bila ya gharama, kwa kuwapo tozo hususani kwa wahitaji wa upasuaji.

Mkuu huyo wa TGNP Mtandao, anasisitiza kwamba wanawake ndio wanaoleta nguvu kazi za kitaifa na hawapaswi kulipa gharama, kwani ili taifa taifa lisonge mbele kuna haja ya kinamama, kuthaminiwa kupitia kazi yao nzito.

Pia upande wa pili analalamika upungufu wa vituo vya afya na zahanati kwenye baadhi ya maeneo vijijini na mijini, ni jambo linalosababisha changamoto kubwa kwa wajawazito, hasa waliofikia hatua ya kujifungua.

Katika angalizo lake, mkuu huyo wa taasisi hiyo ya kijinsia, analalamika bajeti pia haijaainisha kiwango 
ilichojipanga kupunguza upungufu wa watumishi wa afya, kwa baadhi ya vituo vya afya hasa vijijini.

Anatoa mfano kuwapo baadhi ya vituo havina hata huduma za maji na umeme.

MAJI/ MAHITAJI JINSIA

Katika suala la upatikanaji huduma za maji, serikali imefanikiwa kumtua ndoo mama vijijini na mijini kwa asilimia 72.3 na 85 kufikia kukamilika miradi 1845 ya maji, vijijini na mijini. 

Anasema, bado tatizo la huduma ya maji na ugumu wake kwenye maeneo mengi hususani vijijni wanakoshi wanaishi, pia katika mazingira yenye huduma za umma kama vile vituo vya afya na taasisi za elimu.

Lilian anapendekeza serikali kuelekeza Sekta ya Maji kutanua na kuuwezesha mtandao wa huduma za maji safi na salama, kwa kuweka mikakati ya upatikanaji fedha zitakazowezesha suala hilo.

Pia, anaitaka Sekta ya Maji iondoe tozo za maji kwa taasisi za umma kama shule na vituo vya afya na wizara itoa maelekezo kwa idara za maji za mikoa kuwezesha upatikanaji maji kwa wajane na wazee, kwa tozo zenye viwango vya chini, au pasiwapo tozo, hali hiyo ifike hadi pasipo gharama.

Lilian anasema katika kumkomboa msichana shuleni, bajeti imeendelea kuwa kimya katika upatikanaji wa taulo za kike na miundombinu ya hedhi salama kwa wanafunzi wa kike, walio kwenye elimu ya msingi na sekondari.

Anasema bajeti haijataja mafungu au kutoa maelekezo yoyote kwa halmashauri za wilaya, au mamlaka za elimu kuyazingatia mahitaji hayo.

"Katika mafungu ya fedha wanayopata. Kuna umuhimu wa serikali kutoa maelekezo  ya kuwezesha upatikanaji 
wa bajeti hii, ili kuwasaidia wanawake na watoto wa kike kuondokana na fedheha na changamoto za kiafya 
wanazokutana nazo, wakiwa katika hedhi kwa kukosa vifaa safi na salama vinavyojisitiri wakiwa katika hedhi," anasema.

Anaendelea kutoa wito kwa usawa wa jinsia, kwa kuondolewa tozo katika miundombinu ya hedhi salama  kwa wanafunzi wa kike, walio na mfumo wa elimu ya msingi na sekondari.

Lilian anasema bajeti haijataja mafungu au kutoa maelekezo kwa halmashauri za wilaya, pia mamlaka za elimu kuyazingatia mahitaji hayo katika mafungu ya fedha wanayopata. 

Angalizo lake lingine ni katika umuhimu wa serikali kutoa maelekezo ya kuwezesha upatikanaji wa bajeti kuwasaidia wanawake na wasichana kuondokana na fedhea za kiafya wanazokutana nazo, wanapokuwa katika hedhi, hasa kukosa vifaa safi na salama vya kujistiri.

Mama huyo anasema, wanaendelea kutoa wito kwa iliyoko madarakani, wanayoitaja inatambua usawa wa kijinsia wakiitaka iondoe tozo ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye pedi ilirudishwa mwaka 2019.

Lilian anaeleza kwamba, kuna haja ya serikali kutenga bajeti inayolenga kuhamasisha utoaji kwa wajane, wazee na wanawake na kaya maskini nchini.

Anasema,kwa sasa wanaikumbusha serikali kuhimiza makubaliano ya Abuja, Nigeria iliyoridhia haja ya kila serikali kutenga asilimia 15 ya bajeti kuu, kwa jili ya huduma ya afya. 

"Tunatoa wito kwa serikali na wadau wengine kuongeza  uwekezaji katika kutoa elimu ya umuhimu na namna ya kuzuia magonjwa, ili kupunguza gharama za matibabu ya magonjwa yanayozuilika," anasema.

Habari Kubwa