Kwa nini Saratani nyingine ni 'hatari'

24Apr 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Kwa nini Saratani nyingine ni 'hatari'

UTAFITI umevumbua kwa nini baadhi ya maradhi ya saratani ni hatari kuliko aina nyingine ya saratani, ingawa yote yanaonekana kufanana.

Unene wa aina hii ni wa ugonjwa wa saratani.PICHA: MTANDAO

Taasisi ya wanasayansi ya Francis Crick, ilianzisha uchambuzi wa historia ya saratani kwa ajili ya kutabiri mustakabali wake.

Utafiti kwa wagonjwa wa saratani ya figo unaonyesha kuwa baadhi ya uvimbe ''ni hatari'' huku mwingine ukiwa hauna madhara na wakati mwingine hauhitaji matibabu.

Taasisi ya utafiti wa Saratani ya Uingereza (Cancer Research) imesema utafiti huo utasaidia wagonjwa kupata uangalizi mzuri wa kitabibu, kwa kutofautisha kati ya wanaohitaji tiba na wasiohitaji.

Unasema mtu mmoja mwenye saratani anaweza kufa haraka kuliko mtu mwingine mwenye saratani inayofanana ambaye anaweza kuishi kwa miongo kadhaa baada ya matibabu.

Kazi ya utafiti huo iliyochapwa kwenye jarida la Journal Cell, iliainisha saratani za figo kwa wagonjwa 100.

Unazidi kubainisha kuwa wakati saratani inapokua huwa inabadilika zaidi na hatimaye sehemu mbalimbali za uvimbe hujiunda kwa namna mbalimbali.

Unasema ili kuubainisha kinachofanyika ni kwamba watafiti huchukua sampuli kutoka sehemu mbalimbali za uvimbe huohuo na kutazama ni kwa namna gani zina uhusiano wa karibu.

Michael Malley, 72, kutoka jiji la London, alishiriki kufanyiwa vipimo vya ugonjwa huo kwenye hospitali ya Royal Marsden baada ya kugundulika kuwa na saratani ya figo, anasema:

“Kwa kweli tafiti kama hizi ni muhimu kwa ajili ya kupata uelewa ni jinsi gani saratani ya figo inavyokua kadri muda unavyokwenda, na nina matumaini kuwa hii itasaidia wagonjwa kama mimi kupata tiba nzuri,” anasema.

Bado kuna changamoto ya namna nzuri ya kutibu kila aina ya uvimbe, pia namna ya kufanya uchunguzi kwenye hospitali badala ya maabara za utafiti.

BBC

 

Habari Kubwa