Kwanini vidonge vya uzazi vya kinababa ni bidhaa adimu ?

08Apr 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Kwanini vidonge vya uzazi vya kinababa ni bidhaa adimu ?

MIAKA ya 1800 wakati dunia inakumbwa na mabadiliko ya kijamii na uchumi, ongezeko la watu lilidhaniwa kuwa tishio kwa uhai wa binadamu na mazingira yanayomzunguka.

Dawa za uzazi. PICHA ZOTE: MTANDAO.

Wakati huo, mataifa yaliyoendelea yalibuni njia ya kupunguza idadi ya watu, kwa kuhofia siku moja watu wangeshindwa kupata mahitaji yao muhimu kama chakula, elimu na mavazi kutokana na kushindwa kuwamudu.

Hapo ndipo kunaelezwa kwamba, juhudi ziliaanza kufanyika kutafuta njia nzuri bora za kupunguza idadi ya watu kwa kupanga uzazi, kupitia familia.

Hata hivyo, njia zote zilizopatikana zilishindwa kufikia malengo, baada ya kuonekana zipo kwa ajili ya wanawake pekee, huku wanaume zikiwaacha nyuma.

Mwaka 1960 vidonge vya kwanza vya kupanga uzazi vilibadilisha mtazamo wa ulimwengu wakati kilipoletwa katika jamii mnamo miaka ya 1960.

Hivi sasa, vidonge hivyo vinatumiwa na wanawake wapatao milioni 214 duniani kote na kila mwaka, inatumika takriban Dola za Marekani milioni 18,000 (Sh. trilioni 41.4) kuzinunua.

Zaidi ya miongo sita sasa imepita tangu tangu kuzalishwa vidonge, kuna njia 20 za kupanga uzazi, ambazo Shirika la Afya Duniani (WHO) imeziidhinisha, lakini ni aiba mbili tu zinazoweza kutumiwa na wanaume.

Swali linaloumiza vichwa, ni vipi wataalamu wengi wa afya ni kwa nini katika vidonge hivyo vya uzazi, hakuna vinavyotumiwa na wanaume?

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Profesa Adam Watkins, anasema wazo la kutengeneza vidonge vya mpango wa uzazi kwa wanaume, limekuwapo kwa muda mrefu, kama utengenezaji wa mbinu ya upangaji uzazi kwa wanawake.

Mtaaluma huyo bingwa wa Baiolojia ya Uzazi kutoka Chuo Kikuu cha Nottinghan, Uingereza, anasema ugumu mkubwa unaoukabili mpango huo ni wakati mwanamke anatoa yai moja kwa mwezi, mwanaume hutoa mamilioni ya mbegu kila siku, hivyo ni vigumu kuzuia.

Anasema, hata kama mwanaume atapoteza asilimia 90 ya uwezo wake wa kuzalisha, bado anaweza kurutubisha yai na hiyo ndio inachangia sababu kidonge chenye ufanisi na salama kwa wanaume hakijatengenezwa.

"Nadhani ikiwa haijatengenezwa vyema, imekuwa kwa sababu ya mafanikio ya kidonge cha upangaji uzazi kwa wanawake. Inafanya kazi vizuri na ni bora kwa mtazamo wa kiuchumi,” anaeleza mtaalamu huyo.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Njia pekee ambazo mwanaume anashiriki katika upangaji uzazi inayotambuliwa na WHO, ni matumizi ya kondomu na kinga nyinginezo.

"Kwa sababu tofauti, mzigo wa upangaji uzazi ulitwika wanawake,” anaongeza na kufafanua, kwamba wanawake pekee ndio wanawajibika katika jukumu hilo, hatua ambayo wengi wanaona sio sawa.

UHALISIA ULIVYO

Mpango wa uzazi wa zamani katika historia ni kondomu, hii ilianza kutumika miaka mingi na katika karne ya 18, hatua ya mwisho katika mchakato wa kutafuta mbinu ya kiume ya kupanga ilipatikana. Utaratibu wa upasuaji unaokata uwezo wa uzalishaji.

Halafu, katika nusu ya pili ya karne ya 20, baada ya hatua kubwa kupigwa katika utengenezaji wa kidonge cha wanawake, safari ya kutengeza kinachotumiwa na wanaume ilianza, lakini bado inawaumiza vichwa wanasayansi hao.

Njia ya pili inatajwa ni kuzuia mbegu za kiume zenye afya kuingia ukeni na kuweza kurutubisha yai .Hata hivyo, tafiti zinazolenga kubuni kidonge cha kiume zimeathiriwa na changamoto nyingi, ikiwamo zinazosababishwa na viungo vyake.

WANAUME WAJARIBIWA

Mwaka 2016, kuna utafiti uliofanyika kuliwadunga wanaume sindano za ‘testosterone’ na ‘projestojeni’sawa na homoni zilizopatikana kwenye kidonge cha kike, lakini ilipigwa marufuku mapema .

Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya kubainika kukuwapo na athari kama vile chunusi kwenye ngozi, shida za mhemko na wanaume waliona ni kali sana na haiwezi kuvumilika, kwa hivyo uchunguzi ulifutwa.

"Wataalamu wengi wanaweza kuona athari hizi kama ndogo ikilinganishwa na zile zinazopatikana kwa wanawake wanaotumia kidonge, pamoja na wasiwasi, kuongezeka kwa uzito, kichefuchefu, maumivu ya kichwa, kupunguza libido na kuganda kwa damu,” anasema Profesa Watkins.

Kondomu inatajwa hutumiwa sana na wanaume, lakini haina ufanisi kama vidonge na Dk. Lisa Campo-Engelstein, Mkurugenzi wa Taasisi ya Maadili na Afya ya Binadamu katika Chuo Kikuu cha Texas, Marekani, anasema kukosa kidonge cha kupanga uzazi kwa wanaume, sio kushindwa sayansi ya kupata kidonge hicho.

"Ni wazi kwamba kutokuwepo kwa kidonge cha wanaume cha kupanga uzazi sio kwa sababu ya suala la kisayansi, lakini kwa ajili ya suala la kijinsia, la kanuni za kijamii. Kazi hii ilikuwa ya wanawake tu," Campo-Engelstein anasema.

Anaongeza:"Siku hizi wanawake hubeba mzigo mkubwa wa kifedha na kiafya unaohusiana na upangaji uzazi. Kwa ujumla, njia za kike huwa za bei ghali zaidi kuliko za kiume kwa sababu nyingi zinahitaji kumuona daktari zaidi ya mmoja na nyingine zinahusisha dawa zinazofaa kumezwa kwa kipindi fulani,”

Dk. Engelstein anatoa wito wa kuwapo kwa kidonge cha kupanga uzazi kwa wanaume hivi karibuni ili kuwaepusha wanawake kubeba jukumu hilo zito.

Kwa mujibu wa BBC.

Habari Kubwa