Makazi ma4 ya  Fellaini Januari

04Dec 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Makazi ma4 ya  Fellaini Januari

BILA shaka muda wa Marouane Fellaini katika kikosi cha Manchester  United sasa upo mbioni kufikia ukingoni. 

Kwa kiasi fulani Mbelgiji huyo ameonekana kama shujaa wa Old Trafford kwa namna anavyocheza na anavyokuwa mbadala sahihi kwa timu pindi anapohitajika katika nafasi ya kiungo mshambuliaji ama mkabaji. 

Mkataba wa Fellaini unamalizika mwishoni mwa msimu na haionekani kama kuna muendelezo wowote wa mazungumzo uliofanyika katika suala zima la kupewa mkataba mpya, hiyo ikiwa na maana kuna uwezekano wa kuondoka baada ya miaka minne katika klabu hiyo. 

Jose Mourinho ameweka wazi kuwa hataki kumpoteza kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30 kwa sasa, lakini suala hilo lipo nje ya uwezo wake. 

Na kadri siku zinavyozidi kupita, kuna uwezekano mdogo kwa Fellaini kuvaa jezi za United msimu ujao - lakini ni klabu gani itakayotua kumsajili? 

Hizi ni klabu nne ambazo zinaweza kuinasa huduma ya kiungo huyo akiwa huru...

1. Besiktas'*Fellaini amepokea  simu na alipojibu tu 'hallo'* ..." Njoo Besiktas!" Mbelgiji huyo atakuwa sahihi kwa klabu hiyo ya Uturuki kutokana na aina ya uchezaji wake.

Besiktas imeonyesha nia ya kumsajili, na kwa kumnasa itampa nafasi Fellaini ya kuendelea kubaki Ligi ya Mabingwa Ulaya kuwania ubingwa huo wenye utajiri mkubwa kwa ngazi ya klabu barani humo. 2. EvertonMbelgiji huyo anaweza kurejea Goodison Park na kuisaidia klabu hiyo kurudi katikati ya msimamo wa Ligi Kuu England. 

Fellaini anaifahamu vema klabu hiyo kufuatia kuitumikia kwa miaka mitano kabla ya kutua Old Trafford, lakini kuna hofu kuhusu kurejea kutokana na uwezekano mdogo wa kushinda mataji akiwa katika klabu hiyo. 

Itakuwa kujitia majaribuni, lakini anaweza kushawishika kurudi kuisaidia klabu yake ya zamani kuweza kurejea katika makali yake. 

3. PSGKuna tetesi kuwa tayari PSG imeshampa Fellaini ofa ya mkataba wa miaka minne wa kujiunga na klabu hiyo majira ya joto yajayo. 

Kutua Jiji Kuu la Ufaransa, labda kunaweza kuwa vigumu kwake, kutokana na uwezekano mdogo wa kuweza kuwa na kiwango thabiti kutokana na uwapo wa mastaa katika klabu hiyo. 

Kujiunga na PSG kutakuwa na maana kwamba ataweza kuendelea kutwaa mataji, lakini atahitaji kupewa muda wa kucheza mara kwa mara ili kupata mafanikio hayo. 4. NewcastleKadhalika, kama ilivyo kwa Everton, Fellaini kuwa na uwezekano wa kukosa nafasi ya kutwaa makombe, ndivyo itakavyokuwa endapo atatua St James' Park, lakini uhamisho huo utashuhudiwa akiwa mchezaji muhimu katika kikosi hicho cha Rafa Benitez. 

Mbelgiji huyo atapewa majukumu ya namba 10, na wakati huu 'Magpies' hao wakikaribia kuwa mikononi mwa wawekezaji wapya, watakuwa wakihitaji kuwa na wachezaji zaidi kama Fellaini ili kuisaidia klabu hiyo kuwa katika nafasi za juu. Lakini hakika itakuwa ni kujitia majaribuni kwa mara nyingine kwa kiungo huyo.

 

Habari Kubwa