Malipo kwa njia ya simu yaongeza fursa za kujiajiri mtandaoni

03Apr 2022
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Malipo kwa njia ya simu yaongeza fursa za kujiajiri mtandaoni

​​​​​​​WANAWAKE na vijana nchini Tanzania, kama katika mataifa mengine ya Afrika , wanazidi kujiajiri kwa kufanya biashara mtandaoni kupitia simu za mkononi. Kati ya fursa hizi ni uuzaji wa moja kwa moja ambao ni mfumo rahisi wa biashara unaohitaji mtaji mdogo.

Umaarufu wa biashara za moja kwa moja umezidi kuongezeka hususan Afrika Mashariki kutokana na nchi hizo kuwekeza katika kuboresha miundombinu ya mawasiliano kama vile upatikanaji wa mtandao wa intaneti na minara ya mawasiliano.

“Sekta ya uuzaji wa moja kwa moja barani Afrika leo iko katika hatua ya ukuaji na tasnia hii inakua kwa kasi kwa sababu ya kuongezeka kwa wajasiriamali wadogo wadogo," anafafanua bwana Biram Fall, meneja mkuu wa QNET Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Katika taarifa yake na vyombo vya habari mwishoni mwa wiki, meneza huyo alitangaza uzinduzi wa malipo ya fedha kwa njia ya simu kwa wawakilishi wao nchini Tanzania, Kenya na maeneo mengine ya Afrika.

“Kwa kweli ni vigumu kupata kampuni inayofanya biashara ya moja kwa moja barani Afrika ambayo haina kipengele cha malipo kwa njia ya simu, hivo na sisi sasa tumezindua malipo kwa njia simu kusaidia kukuza biashara za wa wakilishi wetu,” alielezea.

"Mfumo wa biashara za moja kwa moja unatoa ajiri nyingi maana unahitaji mtaji mdogo tu kuanza, jambo ambalo hurahisisha vijana na wanawake kujiajiri," aliongeza.

Kwa upande mwingine, uuzaji wa moja kwa moja unakua kwa kasi kutokana na kuongezeka kwa biashara ya mtandaoni Afrika.

Katika ripoti ya McKinsey inaonyesha kuwa thamani ya soko la mtandaoni Afrika itafikia zaidi ya dola za kimarekani trilioni 2.1 ifikapo mwaka 2025. Ripoti hiyo pia inasema, kwa sasa, zaidi ya asilimia 40 ya Waafrika wote wanaweza kupata aina fulani ya mtandao jambo ambalo linapelekea kuongezeka kwa huduma za mtandaoni.

"Swala lingine lililo pelekea kuongezeka kwa biashara za mtandaoni ni janga la uviko 19,” alisema bwana Fall. Kipindi cha Uviko-19 watu wengi walizuiiwa kusafiri hivo kuanza kufanya biashara mtandaoni badala ya kukutana uso kwa uso.

“Janga hilo lilifanya wasambazaji na wateja kutegemea shughuli za biashara ya kielektroniki ili kukidhi mahitaji yao ya bidhaa," aliendelea kufafanua.

Kufikia 2019, malipo kwa njia ya simu yalikuwa na watumiaji zaidi ya bilioni 1 barani Afrika. Mifumo ya malipo ya simu kama vile M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money na zingine inazidi kukua kwa kasi na biashara nyingi zinajikita kupokea malipo kwa njia ya simu.

Kwa kuzingatia maendeleo haya, QNET, moja ya kampuni kubwa za biashara ya moja kwa moja sasa imezindua malipo kwa njia ya simu, alisema bwana Fall.

Faida kubwa ya kutumia malipo kwa njia ya simu ni urahisi wakuwafikia wateja na kupunguza usumbufu wa kwenda benki au madukani kununua bidhaa.

Kampuni hiyo imezindua malipo kwa njia ya simu imezindua nchini Tanzania, Kenya, Rwanda, Uganda, Burundi, na Ghana na inapanga upanuzi zaidi katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Nchini Tanzania, malipo yanapatikana kupitia kampuni zote maarufu za mawasiliano na simu.

Habari Kubwa