Mawakala Tigo Pesa wasimulia walivyokuza uchumi wao 

22Oct 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Mawakala Tigo Pesa wasimulia walivyokuza uchumi wao 
  • Wasema kuna fursa nyingi hivyo watu wazichangamkie.

Baadhi ya mawakala wa Tigo Pesa wameeleza kuwa kupitia biashara hiyo maisha yao yamebadilika na kupiga hatua sambamba na kuongeza fursa na kuwa wafanyabiashara wakubwa na kuwataka watu kuchangamkia fursa iliyopo katika biashara hiyo.

wateja wakipata huduma kwa wakala wa Tigo pesa. picha: mitandao.

Mbali na huduma ya kutuma na kupokea pesa, huduma ya Tigo Pesa imekuwa huduma kamili ya kifedha kwa kutoa mikopo, bima, kuweka akiba pamoja na kupokea pesa kutoka nje ya nchi jambo linaloifanya kuongeza wigo wa fursa kwa mawakala wake.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Mawakala hao ambao wana uzoefu wa kati ya miaka mitano na saba kwenye huduma hiyo wamesema bado kuna fursa kupitia huduma hiyo inayokua kwa kasi hapa nchini.

Suleiman Hussein kutoka visiwani Zanzibar akipokea mfano wa hundi baada ya kuibuka mshindi. 

Suleiman Hussein kutoka visiwani Zanzibar ambaye amefanya kazi ya uwakala kwa kipindi cha miaka saba anasema kuwa kupitia Tigo Pesa ameweza kuimarisha kipato chake kwa kiasi kikubwa ikiwamo kumuwezesha kununua gari mbali na kuendesha familia yake.

“Nashukuru Mungu kupitia Tigo Pesa kipato changu kimekua na nimeweza kununua gari langu pamoja na kuendesha familia yangu.Naona kuna fursa kubwa sana kwenye huduma hii ya Tigo Pesa na ndio maana naendelea kukuza mtaji wangu, kuhudumia wateja wengi zaidi kwasababu ni huduma inayohitajika kila siku,” amesema Hussein.

Hussein anawahimiza mawakala wengine kuboresha zaidi utoaji wa huduma hiyo ili kuweza kuvutia wateja na kuwataka wateja kutumia zaidi huduma za Tigo Pesa katika shughuli zao za kila siku.

Vicky Ibrahim, wakala wa Tigo Pesa Kariakoo.

Naye, Vicky Ibrahim wakala wa Tigo Pesa katika maeneo ya Kariakoo – Msimbazi jijini Dar es Salaam anasema tangu ameanza kazi hiyo ya uwakala miaka mitano iliyopita ameona mabadiliko makubwa kiuchumi licha ya kuanza na mtaji kiduchu.

“Nilianza na mtaji mdogo sana wa laki sita (600,000/-) ila kwa sasa namshukuru Mungu umezidi kukua siku hadi siku.Kuna mafanikio mengi sana nimezidi kuyapata katika kazi zangu kwanza familia yangu imezidi kunufaika kwa kiasi kikubwa.” amesema Vicky.

Anasema siri kubwa ya ukuaji huo ni utoaji wa huduma zenye kuzingatia uaminifu na ubora kwa wateja jambo ambalo linawafanya kuzidi kufika katika ofisi yake.

“Wale ambao wanatarajia au wanataka kuwa mawakala nawakaribisha kwa mikono miwili kwani mimi nilianza na msingi mdogo sana lakini saizi nimepata mafanikio makubwa kupitia hii kazi ya uwakala wa Tigo Pesa,’ amesema.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tigo Pesa, Angelica Pesha anasema kuna fursa nyingi zinazopatikana kupitia uwakala wa Tigo Pesa kwakuwa kwa sasa huduma hiyo imekuwa huduma kamili ya kifedha.

“Tigo Pesa ilianza kama huduma ya kutuma na kutoa pesa ila kwa sasa ni huduma kamili ya kifedha tunatoa mikopo,tunatoa bima ya matibabu kwa mtu na familia na pia tunawawezesha wateja wetu kuweka akiba.Pia, tunawezesha makampuni kufanya malipo mbalimbali kwa urahisi na usalama zaidi,” amesema Pesha.

Pia, huduma ya Tigo Pesa imeingia katika huduma za fedha kidigitali kupitia App ya Tigo Pesa ambayo inampa mteja uwezo wa kutuma na kupokea pesa na pia kurudisha muamala uliokosewa kwa urahisi zaidi.

“Napenda kuwahamasisha mawakala wetu kuendelea kufanya kazi na Tigo kwani fursa bado ni nyingi na pia tunaendelea kutafuta mawakala na kwa wateja wetu waendelee kufanya miamala na Tigo kwani Tigo Pesa ni zaidi ya Pesa,” amesema Pesha.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tigo Pesa, Angelica Pesha.

Habari Kubwa