Mazoezi Yoga sasa hatari kwa afya

07Nov 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Mazoezi Yoga sasa hatari kwa afya

MAZOEZI ya viungo vya mwili, hivi sasa inashika kasi duniani. Washiriki wake wakiwa wa idadi ya mamilioni, hasa kupitia mchezo wa Yoga, ambao pia unaendana imani katika baadhi ya jamii.

Mtu akifanya mazoezi ya Yoga. PICHA: MTANDAo

Kiafya, Yoga manufaa yake inatajwa pia inajumuisha kuuweka mwili kwa usawa. Lakini kama usemi unavyonena duniani ‘kizuri hakikosi kasoro’ sasa inatajwa kuwapo walakini kiafya, pindi mhusika anaopojikita zaidi katika mchezo huo.

Mkufunzi na Mtafiti, Benoy Matthews, kutoka nchini Uingereza, anasema sasa kumeonekana idadi kubwa ya kundi katika umma wanaokutwa na madhara kutokana na kushiriki Yoga.

Anasema, kadri mtu anavyojikita zaidi kuvuta na kunyoosha sehemu za mwili, miili yao inaingia katika hatari ya kuathirika, hata wanalazimika kufanyiwa upasuaji wa mwili.

Mkufunzi Matthews, aliyebobea kitaalamu katika masuala ya maozezi ya viungo vya binadamu, anasema hadi sasa kuna kati ya walimu wanne hadi watano walioathirika kiafya kutokana na ushiriki wao katika mafunzo ya mazoezi hayo kila mwezi.

Anasema, katika kundi hilo zaidi ya nusu wanahitaji zaidi ushauri tu, namna ya kufanya mazoezi ili kuondokana na madhara hayo ya kimwili, kwani kuna aina ya mazoezi viungo vinalazimishwa yasiyowezekana, mathalani kujikunja sana katika baadhi ya viungo visivyokunjika.

Habari Kubwa