Mbinu mpya ya kutibu kisukari

07Dec 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Mbinu mpya ya kutibu kisukari

WATAALAMU wa afya nchini Uingereza, wamefanya utafiti na kugundua mbinu mpya katika kutibu maradhi ya kisukari, kwa kupunguza uzito wa mgonjwa na hasa kutokana na mlo wa mafuta.

Sehemu ya madhara ya Kisukari

Hiyo inaelezwa kwamba mgonjwa anatumia wastani wa miezi mitano kupata mlo wenye wastani mdogo wa viinilishe vya mafuta, hivyo inampunguzia uzito.

 

Tayari imeshaanza kuonyesha matokeo chanya, kwa mgonjwa Isobel Murray aliyetumia mbinu hiyo na kuweza kumpunguzia uzito kwa wastani wa kilo 25.

 

Hatua hiyo inaelekeza mgonjwa kuacha kutumia vidonge vya kisukari na tayari wastani wa wagonjwa

298 wamejaribiwa kwa mafanikio.

 

Katika mafanikio yake, mgonjwa huyo anasema amekuwa akila chakula chepesi kisocho na mafuta katika mpangilio maalum uliochukua wiki 17, akiishi kwa kula mara nne kila siku inavyoshauriwa kitaalam na mafaniko yamejitokeza.

 

Licha ya chakula hicho kuwekewa mapungufu ya baadjhi ya viionilishea kwa makusudi maalum, bado imezingatia hitaji la mlo kamili kwa afya ya mwanadamu.

 

Tayari mafanikio hayo ya awali ya kitafiti, yamekwishawasilishwa kwenye jarida la tiba nchini Uingereza kulikofanyika utafiti huo.

 

Mtaaluma Profesa Roy Taylor, kutoka Chuo Kikuu cha Newcastle, Uingereza ana ufafanuzi kuwa mwanzoni hawakuwa na uhakika kama aina hiyo ya kisukari inayotokana na mfumo wa mlo, inaweza kubadilishwa.

 

Lakini hatua ya utafiti na majaribio, umezaaukwli mpya kluhusu mwenendo huo wa kiafya, kutoka hali mbaya.

 

Tahadhari wanayoitoa madaktari hao watafiti ni kwamba pamoja na maafanikio hayo, wanatahadharisha isichukuliwe kuwa tiba kamili, kwani wahusika wakiongeza uzito, kuna uwezekano wa kisukari chao kurudi.

 

Kitaaluma inaelezwa kuwa, kuwepo mafita mengi katika mwili kunachai uzalisjaii wa sukari zaidi mwili, huku homoni zinazozalisha kinga ya inayozuia kiwango sukari mwilini inaopungua.

 

Mtaaluma mwingine Profesa Mike Lean, kutoka Chuo Kikuu Glasgow, Uingereza anasema:" sasa tuna ushahidi wa kutosha kuwa uzito uliopungua kwa wastani wa kati ya kilo 10 na 15 inatosha kudhibiti ugonjwa huu (kisukari).

 

Wastani wa dunia hivi sasa ni kwamba kati ya kila watu 11, mmoja wao anaumwa kisukari na wengi wanasumbuliwa na kile kinachotokana na mfumo wa maisha na mlo.

 

Athari mbaya za maradhi ya kisiklarti ni pamoja na watu uono wa macho na baadji ya viungo vya mwili kushindwa kufanya kazi. BBC

 

 

 

Habari Kubwa