Mbinu za kuuchelewesha uzee

01Sep 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Mbinu za kuuchelewesha uzee

MAISHA hivi sasa yamegubikwa na matumizi ya vitu mbalimbali vinavyolenga kuzuia mwonekano wa kizee. Hiyo ni kwa mujibu wa mfumo wa maisha uliopo sasa.

Baadhi yake ni matumizi ya vipodozi, wengine wananyoa nywele, ili mvi zisionekane.

Vipodozi hivyo vipo vya aina nyingi, kama vile ‘cream’ za kusafisha ngozi.

Hata hivyo, katika utalaam wa kiafya, kunaelezwa kuwapo mbadala wenye nafasi zaidi ambao ni aina mbalimbali ya vyakula.

Pia inaelezwa matumizi ya vipodozi vya kuondoa uzee unaojionyesha kwenye ngozi, si mbadala halisi wwa kutunza ngozi kuanzia upande wa ndani.

Chakula cha kuzuia kuzeeka haraka mbdala muhimu katika kuufanya mwili usizeeke haraka.

Katika kuulinda mwili dhidi ya mionzi ya jua ambayo ni chanzo kikuu cha mistari na mikunyanzi juu ya ngozi, kuna kinga maalum ambayo inapatikana kupitia lishe.

Je, ni vyakula gani vinasaidia kutunza mwonekano wa ujana?

LISHE

Kwanza, kuna vitu muhimu katika chakula vyenye uwezo wa kulinda mwili usizeeke
hraka, ili kudumisha mwonekano wa zamani (ujana) katika mwili.

Hivyo, changamoto hiyo ya mabadiliko ya kiafya katika mwili, unaifanya upewe mahitaji yaliyobadilika kurejesha hadhi ya mwonekano wa zamani ya walau unaofanana nao.

Kuzuia kuzeeka haraka, kunahitaji chakula chenye madini aina ya ‘calcium’ ambayo yanaipa mwili nguvu na hasa kwenye mifupa.

Pia mtu anatakiwa kuupa mwili virutubisho vya aina ya collagen, kwa kupitia lishe inayoifanya ngozi yake isiwe na makunyanzi.

Miaka zaidi ya 60 iliyopita mwanasayansi Denham Harman, aligundua uhusiano mkubwa uliopo kati ya mwili kuzeeka na kemikali aina ya ‘Free radicals’ inayotengenezwa na mwili, ili ufanye kazi zake wa kawaida.

Mwili wa binadamu una uwezo wa kudhibiti madhara yanayotokana na uwepo wa ‘Free radicals’ kwa kiasi fulani.

Inaelezwa kuwa, idadi ikizidi, mwili unazidiwa na madhara mengi hutokea, ikiwamo kuzeeka na kupatwa na magonjwa mengi kama vile kansa, moyo na kisukari.

‘Free radicals’ huongezeka kutokana na matumizi ya vitu kutoka nje ya mwili. Sumu kutoka nje ya mwili zinazozalisha virutubisho hivyo, ni pamoja na hewa chafu inayotoka katika maeneo ya viwanda.

Vyanzo vingine ni moshi wa sigara, maji na vyakula vyenye dawa za kuua wadudu na utumiaji pombe kuzidi kiwango.

Kiwango kidogo cha ‘Free radicals’ kinachozalishwa mwilini, kinaelezwa kwamba kinaweza kudhibitiwa vyema na kemikali nyingine zinazoitwa ‘antioxidants’ ambazo nazo zinazalishwa na mwili.

Hivyo, binadamu anahitaji lishe yenye virutubisho, ambazo zipo za aina nyingi. Zipo zenye Vitamini C na E na kadhalika.

VYAKULA VYA VITAMIN C

Baadhi ya utafiti katika ripoti zake zinaonyesha kuwa, wanawake wenye umri wa miaka zaidi ya 40 wanawake wanaotumia chakula chenye vitamini C walikuwa na mikunyanzi kidogo zaidi na ngozi zao, ikilinganishwa na waliotumia vitamini hizo kwa kiwango kidogo.

Inaelezwa sababu ni kwamba, vitamini C ina ‘antioxidant’ yenye nguvu inayozuia uharibifu wa chembehai na vinasaba (DNA), hivyo kulinda uzalishaji wa collagen ambayo kiafya ni nguzo muhimu ya kulinda ngozi ya mwanadamu.

Binadamu kimsingi, anashauriwa kutumia walau miligramu 75 za vitamini hiyo kwa siku kumsaidia kiafya.

Kwa mfano, mtu anaweza kupata chungwa moja wakati wa kifungua kinywa na piliplili tano za njano ndani ya ‘saladi’ kwenye mlo wa mchana.

Chakula chenye vitamini C kwa wingi ni pamoja na pilipili nyekundu, nyanya, tikitimaji na kadhalika.

CHAKULA CHA PROTINI

Kuna utafiti unaobainisha kuwa, wanawake waliotumia lishe ya protini kwa wingi wna makunyanzi kidogo kwenye ngozi zao. Hiyo ni kwa sababu protini ina viungo muhimu katika ujenzi wa virutubisho vya collagen.

Ili mtu apate protini, anashauriwa kula nyama ya kuku isiyo na ngozi, sehemu nyeupe ya mayai na samaki.

Mtu anapochagua kula nyama ama ng’ombe au nguruwe na hasa ile isiyo na mafuta sana, ina msaada mikubwa kwake.

Lishe nyingine ni soya, ambayo imeonyesha uwerzi mkubwa katika kusaidia kuondoa mistari myembamba ya kweye macho.

SAMAKI WENYE MAFUTA

Samaki wa baharini wenye mafuta, wamebainika kuwa na kiwango kikubwa cha lishe ya ‘Omega-3 fatty acids.’

Hicho ni kitu kinachosaidia kuilinda ngozi kutokana na mionzi ya jua inayodhoofisha collagen.

NAFAKA

Pia matumizi ya nafaka, badala ya vyakula kama vile wali mweupe, mikate inayotokana na ngano nyeupe na nyingine zilizokobolewa una faida nyingi.

Mojawapo ni kuzuia mwongezeko wa insulini katika mwili, ambayo ina madhara ya kuharibu ngozi.

Pia nafaka ni chanzo cha madini aina ya ‘selenium’ inayosaidia kuikinga ngozi, dhidi ya mionzi ya jua.

Inashauriwa kutumia wali wa kahawia (brown rice), shayiri na ngano nzima, ili msili upate madini yatakayokusaidia kulinda ngozi yako.

CHAI YA ‘MCHAICHAI’

Hicho ni kinywaji chenye ‘antioxidants’ nyingi. Unywaji wa vikombe viwili au vitatu kwa siku wa chai hiyo, unaifanya ngozi kuwa nyororo.

Aina hiyo ya chai, inalezwa kuzuia mikunyanzi kwenye ngozi yako.

O Makala hii imeandaliwa kwa msaada wa taarfa za kitaalam kutoka kwenye mtandao.

Habari Kubwa