Messi, 32, aliikosa safari ya Barcelona kuelekea Marekani, ambapo walishinda dhidi ya Napoli, kutokana na kubabiliwa na maumivu ya kigimbi cha mguu.
Na sasa mshambuliaji huyo anaonekana anaweza kuikosa mechi ya ufunguzi ya La Liga dhidi ya Bilbao, na Valverde akisema ni vigumu kumuona nyota huyo akirejea dimbani.
"Yupo katika hatua ya kupona na sijui kama atakuwa tayari mwanzoni mwa La Liga. Inaonekana vigumu," aliuambia mkutano wa wanahabari baada ya kushinda 4-0 dhidi ya Napoli kwenye mechi iliyopigwa Michigan juzi, Jumamosi.
Licha ya kutokuwapo kwa Messi, Barca ilionyesha kiwango bora katika mechi yao hiyo ya mwisho ya kujiandaa na msimu mpya dhidi ya Napoli, Antoine Griezmann akifunga bao lake la kwanza tangu ajiunge na klabu hiyo, Luis Suarez akitupia mawili na Ousmane Dembele moja.