Mgahawa usiotumia umeme na kuingia ‘mtupu’ wafunguliwa

17Jun 2016
Peter Orwa
Nipashe
Mgahawa usiotumia umeme na kuingia ‘mtupu’ wafunguliwa

Leo ni wiki moja tangu kufunguliwa mgahawa wa aina yake jijini London, huduma za zinatolewa kwa mfumo wa asilia, watu wanaruhusiwa kuwa katika mazingira ya ‘utupu.’

Wenye mgahawa huo unaoitwa Bunyadi, anasema kwamba moja ya sababu kuu ya kufungua biashara hiyo ya kihistoria ni kutumia alichokiita ‘Uhuru kamili.’

Mbali na wahusika kuwa katika mazingira hayo ‘tata’, pia mahali hapo hakuna huduma za nishati zilizozoeleka kama gesi na umeme, bali itatumika nishati asilia.

Katika mfumo wa huduma hiyo, pia vyombo vinavyotumika katika kupika na kula ni vya asili, kama vile sahani na mitungi.

Aidha, wateja wanapoingia mgahawani, huombwa kuzima simu ili kujipa uhuru zaidi, kuashira wapo katika mazingira asilia zaidi, kama walivyoishi watu waliokuwapo katika zama zilizopita.

Sera ya mgahawa huo kwa wageni wanapoingia mgahawani ni kwamba wanakaribishwa kuingia katika chumba maalum, iwapo watapenda ili kubadili nguo wanazopenda kuzivaa au kuacha kabisa na kubaki ‘watupu.’

Wateja ndani ya mgahawa wanatumia taa za mishumaa, meza na viti vya mbao na madirisha ya mianzi.

Tangu kutangazwa kuzinduliwa, imeonekna kuvutia kundi kubwa la wateja na hasi sasa wako 44,200 waliopo katika orodha ya wanaosubiri kuhudumiwa mahali hapo, ambayo ni kiwango kikubwa sana kulinganisha na uwezo halisi wa mgahawa.

KAULI ZA WATEJA

Mteja mmoja, Kashan Kafoor, ameandika katika ukurasa wake wa Facebook akitamka:”Pamoja na vyakula mbalimbali, ninavutiwa sana nikiwea na wenzangu kupata kanuni bora zilizoko hapa na wahudumu wake. Ni kanuni inayofaa kwa migahawa mingi ikiifuata.”

Mteja Lizzie West antamka: “Nadhani uzoefu mzima uliopo ni kugonga sindano kichwani, kuanzia chakula na ninachokisimamia. Najisikia nimepumzika, nina raha na huru!”

Mteja James Hayes, anaongeza kuwa sehemu za mgahawa zimegawanywa kwa mianzi ndani ya migahwa na watu wanazungumza mgahawani wakiwa na raha zaidi.

WENYE MGAHAWA

Seb Lyall, ambaye ni mmili wa mgahawa, pia mbunifu wa mradi huo anatamka:”Wazo lililopo ni kuwa na uzoefu wa ukombozi kamili.

“Tunaamini watu wanapaswa kuwa na fursa ya kufaidi na uzoefu wa kutoka usiku bila ya kero yoyote: hakuna kemikali, hakuna rangi za asili, hakuna gesi, hakuna simu na hata nguo mtu akipenda.

“Tumefanya kazi ya ziada kubuni nafasi ambako watu wanazungumza wakiwa bila ya viatu na wako watupu.”

Ni mgahawa una nafasi 42, ambao kila lishe mlo kamili unauzwa kwa bei ya pauni ya Kiingereza 69 ay sawa na Sh.

MUUNDO WAKE

Ndani ya mgahawa kutagawanywa katika sehemu mbili, moja ni wanaopenda kuvaa ngua na wengine wasipenda kuvaa nguo nao watakuwa na chumba chao.

Mmiliki Seb Lyall, anajigamba kuelezea huduma kwamba chakula kinatolewa katika uhalisia wake na kinapikwa katika namna ya kutopoteza uasilia, kutokana na teknolojia iliyotumika, ambayo ni jiko kuni.

USHUHUDA

Mteja mmoja alitoa ushuhuda wake kama alivyohojiwa na gazeti la Independent la Uingereza.

Anasimulia:”Ni kuishi katika mazingira ya aina yake, tukiwa hatuna siku za mkononi. Ni burudani ya aina yake!

“Mgahawa wa Bunyadi uliopo Kusini mwa mto ulikuwa mzuri sana nilipoingia, nikiwa na wageni wangu. Nilikuta baa iliyowashwa taa inayofifia na meza zitokanazo na miti ziliyokatwa, kuta za mianzi na mishumaa inawaka.

“Baada ya kuvua nguo na kuziweka kabatini, mimi na rafiki yangu tuliongozwa kwenda sehemu ya kukaa, tukielekezwa kwenye mgahawa na mhudumu ambaye naye alikuwa ‘mtupu.’

“Ni mahali kwenye hewa (safi) na sehemu kubwa ya wazi,baadhi ya wateja wanachangika na kwingine wametengwa na kuna sehemu ambazo ni za faragha.

“Hakuna yeyote kati yetu aliyeguswa na kikwazo cha bei au kuhofia kukaa pamoja. Lakini simulizi iilishia katika kukaa wawili ‘chemba’ na kwa kweli mwaka huu wa 2016 ni wa utoto wa aina yake. Kulikuwapo kiza cha namna yake.

“Kilichotawala mawazo yetu ni kule kuwa ‘watupu.’ Suala la kula likawa dogo sana katika kipaumbele chetu kwa wakati huo.

“Chakula kilikuwa cha kawaida ikijumuisha vitu mbalimbali na mboga za majani, nyama na samaki waliotoa moshi.

“Vyakula vyote vinahudumiwa katika viti vya sahani za asili za udongo, hakuna kijiko wala vifaa vya kula. Tunarudia nadharia za siku za mwanzo za mwanadamu.

“Mvinyo nao unahudumiwa katika kifa acha udongo.”