Mkimbizi asimulia machungu yake

22Sep 2016
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Mkimbizi asimulia machungu yake

"Hii ni mara yangu ya pili naishi katika makambi ya jumuiya, mara ya pili kukimbia kutoka vita vya wenyewe ili kujilinda mwenyewe. Nini kinanifanya niondoke (Burundi)? Hii inatokana na mwenendo wa baadhi ya watu kuvamia nyumbani kwa wengine, kuwashambulia wasio na waume

Wanaweza kujipenyeza ndani wakiwa na visu. Kabla ya kukuua,wanakubaka kwanza.

Nilipoona mashambulizi hayo, na watu kufa, nilikimbia pamoja na mwanangu mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja.

Sikuwa na nafasi ya kuwapata watoto wangu wote kwa sababu lilikuwa suala la kila mmoja kujiokoa mwenyewe na maisha yake.

Nilipofika katika kambi la Lusenda ( Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo), sikuwa na matumaini. Kitengo cha Umoja wa Mataifa cha Wanawake (UN Women) kilinipa matumaini, motisha na uwezeshaji.

Baada ya muda fulani, nilikuwa mjumbe wa kamati ya kikundi cha wanawake.

Nilipata kazi hiyo ( nikawa nalipwa fedha kiasai fulani ) na kwamba fedha hiyo imenisaidia kurudi huko nyumbani kwenda kuwatafuta na kuwapata watoto wangu niliowakimbia.

Sasa nina watoto wangu wasichana wanne na mvulana mmoja.

Maisha ya kambini ni changamoto nyingine. Wawili kati ya watoto hawa sasa wamevunja ungo. Wanapokwenda kutembea hubaki katika hofu, kwa sababu wakati wowote wanaweza kubakwa. Chakula pia hakitoshi kulingana na mgao ninaoupata.

Ninaishi kwa kulima kidogo mazao ili kupata fedha kidogo.Ninawaza namnagani ya kujinasua katika wimbi hili na kufikia malengo yangu ya kuilisha familia .yangu na kuipa furaha. Furaha huanza na wewe. "
*Imetafsiriwa toka UN Women

Habari Kubwa